Gari la Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka likiwa katika kituo cha polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kugonga punda |
Waziri
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Bukoba kwenda
Dodoma kugonga mnyama punda katika kijiji cha Wendele Wilayani Kahama
Mkoani Shinyang
Walioshuhudia
tukio hilo walisema lilitokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo lenye
namba za usajili STK 5857mali ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
makazi lililokuwa likiendeshwa na dereva Linusi Eliasi (42) liligonga
mnyama punda aliyekatiza ghafla barabarani.
Akizugumza
na Malunde1 blog mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya
amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa waziri Tibaijuka
alipata mshtuko baada ya ajali hiyo na ofisi ya mkuu wa wilaya Kahama
ilimpatia usafiri mwingine kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya bunge
kufuatia gari lake kuharibika.
Hata
hivyo mkuu huyo wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya amesema waziri
Tibaijuka hakuumia katika ajali hiyo na leo ameendelea na vikao vya
bunge mkoani Dodoma.
Akielezea
zaidi kuhusu ajali hiyo kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga
Kihenya Kihenya amesema Waziri Tibaijuka alikuwa na baadhi ya
wanafamilia wake katika gari hilo wakitoka Bukoba kwenda Dodoma kwa
ajili ya kuwahi shughuli za Bunge zinazoendelea.
Kamanda
Kihenya amesema baada ya kufika katika eneo hilo alikatisha punda
katikati ya barabara na katika harakati za dereva kumkwepa ndipo gari
hilo lilipomgonga na kisha mnyama huyo kufa papo hapo.
Kihenya
alisema kuwa katika ajali hiyo hakuna mtu aliyeumia ila kuna baadhi ya
watu waliopata majeraha madogo madogo ikiwa ni pamoja na waziri huyo
aliyepata mshtuko kidogo lakini baadaye hali yake iliendelea vizuri.
Hata
hivyo katika hali ya mshangao wa watu waliomiminika katika Hospitali
ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya kumjulia hali waziri na kumpa pole
lakini Waziri huyo na msafara wake walikuwa wakipatiwa matibabu na
wauguzi katika Hoteli moja iliyopo pembeni mwa hospitali ya Wilaya
Kahama.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog -Shinyanga
0 comments :
Post a Comment