WAHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamegoma kusimamia mitihani
ya mwisho wa muhula iliyokuwa ifanywe na wanafunzi wa chuo hicho kuanzia
leo wakidai malipo yao ya muhula uliopita yaweze kukamilishwa mara moja
ili kuendelea na kazi.
Aidha, baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao walitegemewa kufanya mitihani ya kumaliza Elimu ya Juu chuoni hapo wamelalamikia mgomo huo kwani wameathirika kutokana na maandalizi waliyokuwa wamefanya kuvurugika na kushindwa kupata muafaka wa sakata hilo.
Mwandishi wa FikraPevu ameshuhudia wanafunzi wa chuo hicho leo Juni 16, 2014 wakirandaranda katika maeneo tofauti ya chuo hicho kufuatila kushindwa kupata muafaka wa kufanya mitihani yao ikiwemo wanafunzi wa Kitivo cha Sheria upande wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
Wamesema kuwa wanasikitishwa kuona hakuna wanafunzi ambaye amefanikiwa kufanya mtihani hiyo, kutokana na mgomo huo, licha ya ratiba ya mitihani kupangwa kuanza leo Juni 16, 2014 saa mbili asubuhi hadi jioni.
Kwa upande wake Rais wa serikali ya Wanafunzi chuoni hapo, Masatu Kiambwene, akizungumza na FikraPevu chuoni hapo alisema “Sisi hatuwezi kuuita huu kuwa ni mgomo kwa walimu bali tunajua wapo kwenye kikao kuanzia mda ule wa asubuhi hadi mda huu wa jioni labda tusubiri baade wakitoka tutajua kuwa ni nini cha kufanya kwa maana wanafunzi wengi sana wameathiriwa na hali ya kutofanya mitihani yao”.
Alisema kuwa, takribani wanafunzi 2000 wameshindwa kufanya mitihani yao mbalimbali ya kuhitimu mafunzo husika na wengine mitihani ya kumaliza muhula, ambapo amedai kuwa, kama hawatapata jibu zuri kutoka kwa waalimu wao hadi saa 12:30 jioni serikali ya wanafunzi italazimika kuingilia kati suala hilo na kutoa tamko.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na FikraPevu wanafunzi hao wamesema kwa ujumla mgomo wa madai ya walimu wao umewaathiri kwa kiwango kikubwa, kutokana na maandalizi waliyokuwa nayo katika kipindi cha muda mrefu.
SOURCE:FIKRA PEVU

0 comments :
Post a Comment