Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha
Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia
kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi
kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye
amefahamika kwa jina la JOSEPH
NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha
aina ya SMG ikiwa na risasi
30.
Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na
kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi
za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.CHANZO MICHUZI BLOG
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu
kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE
amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu
wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega
kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye
VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu
hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili
hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni
kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila
kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako
kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN
0 comments :
Post a Comment