-->

RAISI UHURU KENYATA ASEMA SHAMBULIO LA MPEKETONI LILISABABISHWA NA VUGU VUGU LA KISIASA


Mauaji ya Mpeketo yemesababisha vifo vya watu zaidi ya hamsini
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja kupitia kwa televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku.
Kenyatta emesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema na kwamba wanasiasa walihusika nao.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu jioni.
Alisema kuwa ujasusi ulitolewa kuwa mashambulizi hayo yangefanyika lakini hawakuchukua hatua zozote kuzuia mashambulizi hayo.
Rais amesema kuwa maafisa waliohusika tayari wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa. Wmaesema kuwa wanachunguza wanasiasa waliohusika na mauaji hayo.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa jamii.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment