Kitengo cha kimataifa cha
kupambana na uhalifu kinawataadharisha watumiaji wote wa kompyuta kuwa
wana muda wa wiki mbili kuweza kuhami kompyuta zao dhidi ya mashambulizi
ya hali ya juu katika kompyuta hizo.
Hili limekuja mara baada ya maafisa wa kimarekani kufanya mkutano na waandishi wa habari wakimtuhumu mwananchi wa nchi ya Urusi kwa kuendesha uhalifu huo unaokadiriwa kufikia Pauni milioni 60.
Aina mbili za program mzunguko ambazo ni GOZeuS na CryptoLocker ndio hasa zinazolengwa katika tahadhari hii.
Watu wanapewa tahadhari kuhakikisha kwamba program zao za ulinzi (Antivirus) na zile zinazoendesha kompyuta (Operating System) vinakwenda na wakati na wacheki mara kwa mara iwapo kompyuta zao zipo salama.
Programu mzunguko inaharibu kompyuta kwa njia ya viambatanisho au njia mpokeo katika barua pepe.
“Njia mpokeo na viambatanisho hivyo vinaweza kuonekana kama vimetumwa na mhusika halisi na kamili ambapo zinakuja kama zimebeba ujumbe wa sauti au file lolote lililotengenezwa katika hali ya kutoweza kutiliwa shaka yoyote,” Kitengo cha uhalifu kinataadharisha.
Barua pepe hizi zinasambazwaa na waathirika wengine bila wao wenyewe kujua kwamba zimeathirika, na huwa wanatuma barua pepe nyingi sana hivyo kuongeza idadi ya watu wanaoathirika na tatizo hilo.
Kitengo cha uhalifu kinasema kwamba GOZeuS ambayo vilevile inajulikana kama P2PZeuS inahusika katika katika kuiba kwa udanganyifu kwa mamilioni ya pauni duniani kote.
Muwasilishaji taarifa wa kituo cha teknolojia cha Sky, Tom Cheshire anasema, tunapaswa wote kuwa waangalifu. Inaenda haswa katika taarifa za fedha, na baada ya hilo kukamilika aina fulani ya mzio inaanza kuiba hizo fedha popole sana bila ya hata mtu kuweza kugundua.
Tishio la pili linatoka katika program mzumguko ya Cryptolocker, ambayo huwa inaamshwa baada ya tishio la kwanza hapo juu kuwa halijatengeneza faida ya kutosha.
Hii inamzuia kabisa mtumiaji wa kompyuta asiweze kupata mafaili yake, kwa mfano picha au miziki, na zaidi inatishia kuyafuta kabisa kama kiasi fulani cha fedha hakitalipwa.
Zaidi ya kompyuta 15,500 nchini Uingereza zimeathirika na nyingi zaidi zipo katika hatari ya kuathirika, kulingana na kitengo cha uhalifu.
Stewart Garrick, afisa mwandamizi wa kitengo cha uhalifu amekiambia kituo cha Sky News kwamba tishio hili lililenga zaidi watu binafsi na mifumo ya kompyuta ya kiutendaji ya biashara.
Tishio hili halibagui kabisa, halijalishi ni kompyuta gani inavamia tu.
Tishio hili lipo kwa matumizi ya wahalifu kuvuna pesa moja kwa moja kutoka katika akaunti za benki, au kushinikiza kupata malipo ili mtu aweze kupata mafaili yake.
Mrusi Evgenil Bogachev (30),anashutumiwa kuwa kionngozi wa kundi la uhalifu linalohusika na uhalifu huu, Mkurugenzi msaidizi wa FBI Robert Anderson amewaambia waandishi wa habari Washington DC.
“FBI wameweza kuvuruga mtandao huu na kuuhodhi,” Tom Cheshire wa Sky anasema.
Hivyo pale wahalifu watakapojaribu kuwasiliana na kompyuta ambayo imeathirika, njia hiyo ya mawasiliano imekatishwa.
Sasa una nafasi ya kusafisha. Kitu cha kwanza unachopaswa kufanya ni kupitia mfumo wa ufanyakazi wa kompyuta mara kwa mara hasa zaidi kama upo kwenye windows, alafu angalia kuchuja Kompyuta yako kwa ajili ya kuondoa virusi ambapo utakuwa na nafasi ya kuweza kuvipata.
0 comments :
Post a Comment