WENGI
wetu tungependa kujua historia ya vidonge vya lishe au lishetiba au
Food Supplement kama inavyojulikana kitaalamu na nani aliyeanzisha
utaratibu huu duniani wa kukigeuza kidonge kuwa chakula.
Kabla
ya mwaka 1934 hakukuwepo lishetiba ya aina yoyote duniani kitu ambacho
kiliwafanya watu wa enzi hizo wapate wakati mgumu lilipokuja suala la
kuboresha afya zao pale palipokuwa na upungufu wa virutubisho mwilini.
Mwaka 1934
mwanasayansi aitwaye Carl Rehnborg alianzisha kampuni ya Nutrilite kwa
ajili ya kutengeneza lishetiba. Kampuni hii imeendelea hadi leo na kuwa
miongoni mwa makampuni makubwa ya kutengeneza virutubisho duniani.
Kampuni hii ndiyo inayotoa udhamini mkubwa kwa timu ya mpira wa miguu
maarufu nchini Italia ya A.C.Milan.
Haikuwa kazi
ndogo kwa Rehnborg kufanikiwa kuanzisha kampuni hiyo, bali yalikuwa ni
matunda ya jitihada na tafiti mbalimbali za tangu mwaka 1920 wakati
akiishi nchini China akiwa askari jeshi ambapo aligundua kuwa kulikuwa
na uhusiano mkubwa sana kati ya maradhi hasa yale sugu na vyakula
wanavyokula wanadamu.
Kikubwa
kilichomshtua ni kuona kuwa jamii ya wakulima ambao walikula matunda na
mboga kwa wingi walikuwa na afya njema huku jamii ya watu walioishi
mijini ambako matumizi ya mafuta, sukari na chumvi ni makubwa, walikuwa
wakisumbuliwa na maradhi sugu mara kwa mara.
Carl alipata
wazo la kuchanganya virutubisho alivyohisi kukosekana katika vyakula
walivyokuwa wakila jeshini. Alichanganya dawa za asili, aina fulani za
majani na mboga, chokaa na unga wa misumari (ili kupata madini ya
chuma), pamoja na unga wa mifupa (ili kupata madini ya Calcium) na
baadaye alikula mchanganyiko huo na baadhi ya wanajeshi wenzake.
Japo ladha
ya mchanganyiko huo haikuwa nzuri, lakini waliokula baada ya muda mfupi
walianza kunawiri na afya zao kuimarika tofauti na waliokula chakula cha
jeshi cha kawaida.
Baada ya
miaka kadhaa, Car alirejea nchini Marekani na kuanzisha maabara yake
ndogo katika Kisiwa cha Balboa ambapo baada ya miezi sita tu akawa
ameshafanya majaribio na kugundua lishetiba nyingi sana kwa kutumia aina
nyingi tofauti za mimea na wanyama.
Pia
aligundua namna nyingi za kukausha na kuhifadhi bidhaa hizo bila
kuathiri ubora wake wa asili na alizalisha bidhaa za lishetiba kwa wingi
zenye vitamin, madini na tindikali mbalimbali kulingana na mahitaji ya
mwili wa binadamu. Hadi leo kampuni yake ya Nutrilite ndiyo inaheshimika
sana duniani kama mwanzilishi wa lishetiba chini ya uongozi wa mwanaye
Dr. Sam Rehnborg.
Baadaye,
kampuni nyingine nyingi zikaibuka ikiwemo kampuni kubwa nchini Marekani
iitwayo Herbalife inayomdhamini mchezaji bora duniani Christiano Ronaldo
anayekipiga timu ya Real Madrid ya Hispania, inadaiwa kuwa afya ya
Ronaldo ni imara kutokana na kutumia virutubisho kwenye mlo wake.
Nchini
Tanzania lishetiba ni kitu kigeni kidogo na ndiyo maana siyo rahisi
kuzikuta lishetiba kila duka, hospitali au kwenye maduka ya dawa pia
hata sehemu zinakopatikana ni ghali sana kumudu watu wa kawaida.
Hata hivyo,
kupitia safu hii, unaweza kujua aina mbali mbali za tibalishe na mahali
zinakopatikana kwa hapa nchini. Tunawasihi watu wenye uwezo na ambao kwa
njia moja au nyingine wameshindwa kupata na kutumia matunda na mboga za
majani badala yake watumie vidonge vya lishe kulinda afya zao.
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment