Mmmoja miongoni mwa wazungumzaji katika warsha(SEMINAR) iliyohusisha watu 200 alisimama na kuanza kusema huku akiwa ameshika sh 10000 mkononi
Kuna mtu anaipenda hii?aliuliza
watu wote wakajibu kwa nguvu huku wakinyanyua mikono juu....Tunaipendaaaa!!!!!!
Kisha akasema pesa hii nitampa mmoja wenu ila kabla sijampa nitaifanyia kitu hiki.......Akaanza kuikunja kunja kwa mikono yake kisha akasema
Kuna mtu anaipenda hii bado?
Wote wakanyoosha mikono kuashiria wanaipenda
Kisha akasema yaani pamoja na kuikunja kunja bado mnaipenda basi ngoja niifanyie hivi kwanza...
Akaiangusha chini kisha akaanza kuikanyaga kanyaga ikajaa michanga na kuchafuka...Alipomaliza akauliza kuna mtu bado anaipenda hii?
Woote wakanyoosha mikono kuashiria bado wanaipenda
Kisha akawaambia leo mmejifunza kitu bora sana.Pamoja na yote niliyoifanyia pesa hii lakini bado mmekuwa mkiihitajia kwa sababu haikupungua thamani yake kwa kukanyagwa au kukunjwa kukunjwa au kuchafuliwa lakini thamani yake imebaki kuwa vile vile 10000...
Hivyo basi naomba mtambue kuwa katika maisha yetu kuna kipindi tunachafuliwa au kuvulugwa na maisha au misukosuko mbali mbali lakini thamani yetu itaendelea kubaki vile vile...
Kuna kipindi tunajihisi hatuna thamani kutokana na vurugu za maisha au kushindwa kutekeleza ndoto zetu basi TAMBUA THAMANI YAKO NI ILE ILE, YOU ARE SPECIAL
weka mafunzo uliyapata hapo chini
0 comments :
Post a Comment