JESHI la
Polisi mkoani Mwanza, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga waliokuwa wakipinga
kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini
Mwanza. ...
Hatua hiyo
imesababisha vurugu kubwa na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za
kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na
baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara
zinazokatiza katikati ya jiji kuanzia saa nne asubuhi ....
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Valentino Mlowola, amedai kuwa Jeshi hilo limelazimika kutumia mabomu hayo ili kuwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wakihatarisha amani na kwamba hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo.
0 comments :
Post a Comment