Ukitoa
sehemu ambazo umekwisha zisikia kuwa zimegundulika nishati ya Gesi
unaambiwa Kampuni ya Statoil ya Norway na mshirika wake ExxonMobil
wamegundua kiasi kingine kikubwa cha gesi katika Bahari ya Hindi.Kwa
mujibu Statoil wamedai kuwa Kiwango hicho kinakadiriwa kufikia futi za
ujazo trilioni mbili mpaka tatu (sawa na lita trilioni 56.6 hadi
trilioni 84.9).Ugunduzi huu unafanya jumla ya ujazo wa gesi
iliyogunduliwa na washirika hao kufikia takriban futi za ujazo trilioni
20 (lita trilioni 566.25) kwenye Kitalu Namba 2, ambako washirika hao
wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji.
Makamu wa
Rais kwa shughuli za utafiti wa Statoil ukanda wa Magharibi ndugu Nick
Madem amesema>>’tangu mwaka 2012 tumekuwa tukipata mafanikio ya
asilimia 100 nchini Tanzania na eneo hilo limekuwa kitovu cha utafiti
ndani ya muda mfupi’
Nick
Madem ameongeza kwa kusema>>’Ni kwa haraka tulitoka kwenye
kuchimba kisima kimoja hadi kuwa na mkakati wa kuchimba visima vingi’.
Ugunduzi
huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango
kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi
katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012.
Ugunduzi
katika kisima hicho unakuwa wa sita katika Kitalu Namba 2,uchimbaji wa
gesi katika kisima hicho ulifanywa na meli ya Discoverer Americas,usawa
wa mita 2,360 za kina cha maji. Meli hiyo sasa inachimba kisima kingine
cha Binzari katika Kitalu namba 2.
Statoil
ambayo imekuwapo Tanzania tangu mwaka 2007 ambao wamkua wakifanya
utafiti na kuchimba gesi katika kitalu namba 2 kwa niaba ya Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na hisa ya asilimia 65 katika
kitalu hicho wakati ExxonMobil Exploration and Production Tanzania
Limited ina asilimia 35.
Source:Mwananchi.
0 comments :
Post a Comment