Mkurugenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa mamlaka hiyo, Dk Joseph Kilongola.
Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta utakaoratibu taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya uandishi wa habari.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta utakaoratibu taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya uandishi wa habari.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa teknolojia ya
habari na mawasiliano wa mamlaka hiyo, Dk Joseph Kilongola katika
kongamano la kimataifa la habari lililo andaliwa na Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) na kufanyika jijini hapa kwa mara ya kwanza, mwaka huu.
“Licha ya kuwaelimisha wadau wa habari hasa
wamiliki wa ‘blog’ juu ya kuzingatia maadili ya uandishi kwa kila
wapakiacho mtandaoni, sasa tunakuja na cyber security itakayosimamia
upashanaji habari,” alisema Dk Kilongola.
Alisema mfumo huo utafanya pia kazi ya kuchuja
habari zote kabla hazijawekwa mtandaoni na utatoa ulinzi kwa jambo
lolote linalotishia usalama katika sekta yoyote ya uchumi na kabla
madhara hayajatokea, wahusika watakuwa wameshajulikana.
Profesa Florens Luoga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) alitahadharisha dhidi uhuru na haki ya matumizi ya
majukwaa mbalimbali ya mawasiliano kuwa yanapaswa kuzingatia maadili ili
kuepusha athari zinazoweza kujitokea katika jamii.
“Kila teknolojia mpya huja na athari zake.
Maendeleo ya teknolojia ya habari nayo yamekumbwa na hilo. Athari zake
zimeanza kujitokeza.
“Maadili ya kitaaluma ni vyema yakazingatiwa na
wote wanaojihusisha na upashanaji habari ili kuchangia maendeleo
yaliyokusudiwa,” alisema Profesa Luoga.
Alihimiza wataalamu wa habari kuhudhuria makongamano ya kitaaluma yanayoandaliwa.MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment