Na Dk. Chale
MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika
katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary
Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna
hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke anayo historia kama
alishawahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au
iliharibika.
Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au ugumba.
Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.
Maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na magonjwa sugu pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.
Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanamke
Vyanzo
vya matatizo haya vinahusisha aina zote mbili za ugumba za ‘Primary’ na
sekondari’. Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai
‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo
mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai.
Hii
husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza
kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi
yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi
ya vyakula au vipodozi, tutakuja kuona.
Katika makala zijazo
Dalili
za upevushaji wa mayai zipo nyingi, tutakuja kuziona hapo baadaye
lakini kubwa ni kwa mwanamke kupata ute wa uzazi ambapo upo wa aina
tatu.
Pia upevushaji tunaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu
ambavyo unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi
unaweza kupata mimba.
Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye
mirija, mirija inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji.
Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga
kizazi.
Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni
husababisha athari katika kizazi na mirija. Matatizo ya mirija
husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi
40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.
Mwanamke
pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi ambapo
linatoka kwa nje badala kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa
‘Endometriosis’. Siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini
linaathiri baadhi ya wanawake.
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika
maumivu chini ya tumbo na huwa makali wakati wa hedhi na kusababisha
damu ya hedhi kutoka kidogokidogo, mwanamke hupoteza uwezo wa kushika
mimba.
Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa,
anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume
ambao humuathiri mwanamke. Mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa
vizuri, anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa.
Mwanaume
anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa
mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vema naye akafanyiwa
uchunguzi endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya
mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina
inaonekana mume hana tatizo wala mke hana tatizo, hali hii inaitwa
kitaalamu ‘Unexplained Inferlity. Kwa hiyo, ni vema uchunguzi wa kina
ufanyike. Tatizo hili tutakuja kuliona katika makala zijazo.
Uchunguzi
Matatizo
ya ugumba ni makubwa na huumiza vichwa vya watu wanaotafuta ujauzito.
Tumeona sababu kuu za ugumba lakini mambo mengine yanayohusiana na
lishe na magonjwa sugu yanayoathiri uzazi. Tutakuja kuzungumzia.
Uchunguzi
hufanyika kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi
katika hospitali za mikoa na wilaya. Vipimo mbalimbali hufanyika kama
damu kuangalia viwango vya homoni, ultrasound na mirija uzazi.
CHANZO:GPL
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment