Klabu ya Manchester United imemsajili beki wa kushoto wa Southampton,Luke Shaw kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 30.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 amesaini
mkataba wa miaka minne pamoja na fursa ya miezi 12 zaidi ndani Old
Trafford ambayo imekubalika mara baada ya kurudi kutoka kwenye kombe la
dunia na Uingereza.
Man United walipeleka ofa ya pauni milioni 27
kwa Shaw ambayo ilikataliwa mwishoni mwa msimu uliopita lakini maboresho
ya ofa yamefanikisha lengo.
Nyota huyo ambaye alicheza mchezo mmoja katika michuano ya kombe la
dunia anaungana na Ander Herrera katika kuelekea Manchester;kiungo huyo
anakwenda kwa mkataba wa miaka minne akitokea Athletic Bilbao kwa ada
inayofikia pauni milioni 28.
0 comments :
Post a Comment