Maafisa nchini Afghanistan
wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi
baada ya gari lao kazkazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa
barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi
ya pili.
Katika tukio jengine kundi la Taleban liliwakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
Raia wa taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha.
Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.
0 comments :
Post a Comment