WATU 17
wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha,
kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na
kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.
Watu hao
walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya
Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana
na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi
hiyo.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba
ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini
hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa
namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao
itatajwa tena juni 12
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment