Mwenyekiti wa Yanga SC - Yusuf Manji akiongea na wanachama
wa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi – Oysterbay Mkutano Mkuu wa marekebisho ya
baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na
furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha
kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza
wanachama hai wapatao 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya
maslahi na faida ya Wana Yanga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza
kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.Aidha katika mkutano huo Manji
amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa usajili unaendelea kufanyika na
nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi utakapokamilika basi wataweka wazi kila
kitu.Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi
mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi
kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume
aliongoza kikao cha waachama kilichomuomba Bw Manji kuendelea na uongozi ambapo
mwenyeikti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na pindi waliporejea
walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za kikatiba.Mwisho kupitia
mkutano mkuu wa leo wa wanachama umeazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja
Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze
kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya
katiba kupitishwa na TFF.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu akisoma mapendekezo ya
kipengele cha Kamati ya Maadili kwa wanachama
0 comments :
Post a Comment