-->

VIJANA WABUNI MRADI WA KUTENGENEZA DARAJA MWEMBESONGO NA KUJIINGIZIA KIPATO


Shomari Ramadhan kulia na Paschal Greygory wakiwa katika usimamia wa utozaji wa ushuru wa daraja walilojenga kwa miti katika barabara kuu ya Kichangani-Mwembesongo kufuatia mvua za masika zilizosababsiha mafuriko kuharibu miundombinu ya barabara na kukatika kwa mawasiliano Manispaa ya Morogoro, jumla ya vijana saba wametumia fursa hiyo kwa kujenga daraja baada ya halmashauri ya Manispaa hiyo kushindwa kurejesha miundombinu kwa muda mrefu mkoani hapa.


Na Mtanda Blog, Morogoro.
Mvua za masika zilizonyesha kwa kiwango kikubwa hapa nchini ikiwemo mkoa wa Morogoro, zimetosha kutoa fursa kwa vijana kuweza kupekecha akili na kuondoka na wazo la upatikanaji wa ajira inayowaingizia kiasi cha sh 50,000 hadi sh 60,000 kwa siku kutokana na ubunifu wao wa mradi wa ujenzi wa daraja la miti katika barabara kuu inayounganisha kata ya Kichangani na Mwembesongo mkoani hapa.

Kiwango cha pesa wanachovuna vijana hao kwa siku kinatokana na halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuchelewa kurejesha miundombinu ya barabara ya Mbwembesongo na Kichangani eneo la matofarini iliyokata mawasiliano kabisa baada ya maji ya mafuriko kubomoa sehemu kubwa na magari na pikipiki kushindwa kupitika kutokana na uharibifu huo kwa zaidi ya mwezi sasa.



Uharibifu huo wa barabara kubomoka umesababishwa na maji ya mafuriko yaliyoshindwa kupita katika mto Morogoro eneo la mto Kilakala sababu kubwa ikiwa mto huo kujaa mchanga na maji kupoteza mwelekeo na kuleta madhara katika makazi ya watu kwa nyumba kubomoka na kuharibu miundombinu ya barabara.
Sehemu ya barabara inayounganisha Kichangani na Mwembesongo ikiwa imeharibiwa na maji ya mafuriko kukatikana kwa mawasiliano.


Shomari Ramadhani (37) ni kiongozi wa vijana wenzake sita waliokuna vichwa na kupekecha akili na kubika na mradi wa ujenzi wa daraja la miti ambapo mwanzo wa ubunifu wao ni kupita pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu ikiwalenga zaidi wanafunzi, wazee na walemavu wanaoshindwa kupita katika bonde lenye vikwazo vingi baada ya maji ya mafuriko kuharibu miundombinu ya barabara hiyo.



Aliwataja wenzake waliohusika katika ujenzi wa daraja hilo kuwa ni pamoja na Paschal Greygory, Ally Abdallah, Samuel Rajabu, Omari Mrisho, Juma Athaman na Harouna Saidi.



“Mwanzo baada ya kutokea kwa hali ya mafuriko kuharibu barabara na magari, pikipiki kushindwa kupita katika barabara inayounganisha kata ya Kichangani na Mwembesongo eneo la matofarini tulikaa mimi, Allya na Paschal kuona ni namna gani tunaweza kujenga daraja la miti lakini lengo likiwa kuwatoza waendesha pikipiki kiasi cha sh3,00 huku watembea kwa miguu na baiskeli tukiruhusu kupita bure.”alisema Ramadhan.

Wakazi wa kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro wakijadiliana jambo mara baada ya maji ya mafuriko kuvamia makazi yao huku zaidi ya kaya 150 katika eneo la Kwachuma kupata hasara mbalimbali kufuatia mvua za masika 2014.


Aliongeza Ramadhani kwa kusema kuwa ilibidi wachangishane ili kupata fedha za manunuzi ya vifaa ikiwemo kiasi cha sh120,000 za kununulia magogo ya mnazi, viroba tupu 2,00 ikighalimu sh 20,000 na misumari inchi nne na tano kilo 20 sh 24,000 na kuanza ujenzi ambao ulikamilika kwa siku mbili likiwa na ukubwa wa futi 4.5.



Ramadhan alisema kuwa baada ya kumalizika kwa kazi ya ujenzi wa daraja hilo, pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu walianza kupita kwa pikipiki kutozwa kiasi cha sh3,00 huku magari yakishindwa kupita kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuhimili uzito mkubwa kabla ya kuongeza nguzo na vironga vya mchaanga vilivyosaidia kuimalika na magari madogo kuweza kupita.



“Daraja lilikuwa na upana mdogo wa upana wa futi 3 tu na kuona haja ya kuongeze upana ili na magari nayo yapite lakini tunaruhusu yenye uzito wa tani 10 tu kwani yakipita zaidi ya uzito huo linaweza kutitia ambapo hutozwa sh 5,00.”alisema Ramadhan.



Kutokana na ushuru wanaotoza kutoka kwa pikipiki na magari wamekuwa wakiingiza kiasi cha sh 50,00 hadi sh 60,000 kwa siku na kujikuta wakigawana kiasi cha sh 5,000 hadi sh 6,000 kwa siku na kujiwekea akiba ya sh 10,000 huku wakiwa na jumla ya akiba ya sh 250,000.



Ili kukusanya fedha hizo hulazimika kuanza kazi ya kukusanya ushuru huo saa 12 asubuhi na saa 1 jioni huondoka eneo hilo baada ya saa 1 na kuendelea hupita bure bila malipo.


Mkazi wa kata ya Mwembesongo Athanas Ngozi (59) anaanza kwa kutoa historia kwa kueleza kuwa zamani miaka ya 1960 enzi za mkoloni kando ya mto Morogoro kulikuwa na miti mikavu ya micharaka iliyochimbiwa ardhini na lengo lilikuwa kutoyapa maji nafasi kabisa ya kupoteza mwelekeo zaidi ya kufuata mto.

Ngozi alisema kuwa achilia mbali mto Morogoro kuwekea micharaka kama sehemu ya kuzuia kingo zisiharibiwe na maji katika mto huo hata ule wa Kikalakala nao uliwekewa makaravati kutoka FFU hadi unaungana na mto Morogoro.

“Haya mafuriko ni ya kujitakia sisi wenyewe hasa hawa Manispaa ya Morogoro kwani kama wangefuata kanuni zile za mkoloni za kuhudumia mto Morogoro, Kikundi na ule wa Kilakala pasingekuwa na mafuriko katika makazi ya watu kwani mafuriko hayo yanawakumba wananchi kwa sababu mito yetu haiwajibiki kwa kuifanyia usafi.”alisema Ngozi.

Ngozi aliendelea kufafanua kuwa mafuriko yaliyoikumba Manispaa ya Morogoro yametokana na uzembe wa viongozi ndani ya serikali kwa kuacha kila mtun aliyekando na mto kutupa takangumu kando na kuufanya mto kujaa uchafu na kuwa chanzo cha kujaa mchanga uliosababisha kupunguza kina chake kwa 85% kwa baadhi ya sehemu.

Wakazi wa kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro wakijadiliana jambo mara baada ya maji ya mafuriko kuvamia makazi yao.

 “Sikushangaa kuona vijana saba wa kata ya Kichangani kubuni mradi wa ujenzi wa daraja la miti eneo la Matofarini kama sehemu ya kujitafutia ajira halali kwa kutumia fursa ipasavyo kwa kuwatoza madereva wa magari na pikipiki kwani Manispaa wamechelewa kurejeshea haraka miundombinu ya barabarani iliyoharibiwa na maji ya mafuriko na kukata mawasiliano ya kutopitika kwa magari wala pikipiki.”alisema Ngozi.

Alieleza sababu za barabara hiyo kuharibiwa na maji ya mafuriko kuwa chanzo chake ni maji ya mvua za masika yamesababishwa na maji kubomoa sehemu dhaifu ya makutano ya mto Morogoro na Kilakala kutokana na kuwa na kona iliyochangiwa na matumizi mabaya ya binadamu ndani ya mto huo na kuadhiri makazi ya watu.

“Tumshukuru mungu kwa kutuletea mvua za kutoka mwaka huu lakini kwa upande mungine zimeleta hasara kubwa tu kwa watu na serikali lakini kwa upande wa serikali wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa kuingia ghalama kubwa za ukarabati wa barabara ya Kichangani-Mwembesongo kwani kama wangeufanyia usafi mto Morogoro, maji yasingepata nafasi ya kubomoa kingo zake na hii imetokana na utendaji udhaifu wa viongozi wetu.”alisema Ngozi.

Udhaifu ho kwa viongozi ni kushindwa kuzuia vijana wanaofyatua matofari eneo hilo ambao baadhi ya sehemu wamechimba udongo mita chache na mto huo nalo limechangia wakazi wa Kwamchumba-Kichangani, Mwembesongo mtaa wa Mzambarauni, Kidabaga na Kidebwe kukumbwa na maji ya mafuriko yaliyoshindwa kupita mto Morogoro.alisema Ngozi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Riverside kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, Saleh Luzegea (64) anaeleza kuwa vijana hao wapo sahihi kujenga daraja la miti kisha kuwatoza ushuru madereva wa pikipiki na magari kwani kitendo hicho kimekuwa mkombozi japo kwa kutatua sehemu ya kero kutokana na halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kushindwa kurejeshea miundombinu mpaka sasa baada ya kutokea kwa amfuriko april mwaka huu.


"Hili daraja limekuwa mkombozi kwa wakazi wa Mwembesongo, Kichangani, Areasix, Areafive, Ninja na Nane Nane kwani kabla ya vijana hao kujenga daraja la muda la miti kulijenga baada ya mafuriko kuharibu miundombinu ya barabara hiyo walikuwa wakilazimika kulipia ghalama ya pikipiki kiasi cha sh3,500 badala ya sh 1,000 ya awali kulikotokana na ubovu wa barabara hiyo."alisema Luzegea.


Aliongeza kuwa barabara hiyo ilikuwa ikitumiwa kwa kupita magari makubwa na yale ya abiria kwa miji midogo ya Kisaki, Mkuyuni na Matombo lakini sasa hivi yanashindwa kupita kutokana na adha hiyo na kulazimika magari makubwa yaliyozidi uzito wa tani 10 kuingia Manispaa ikivunja sheria ya katikati ya mji kutoingia magari yenye uzito huo.


Luzegea alisema kuwa amekuwa akifanya usafi chini ya daraja la Mwembesongo kwa kuondoa taka zilizosombwa na maji na kukwama lakini inafikia wakati anashindwa kufanya kazi hiyo kutokana na kukosa vitendea kazi.

Manispaa wanaweza kuanza utaratibu wa kupanda miti kando ya mito yake na kuondoa mchanga ili vina vya mito hiyo view kama zamani na endapo watafanya hivyo ana uhakika hakuna mkazi atayekumbwa na mafuriko kwani sehemu zilizosababisha mafuriko katika mto huo zinapaswa kuonyoshwa ili mto urudi katika asili yake.

Taarifa ya serikali ya mafuriko inaeleza kuwa jumla ya kata sita zimekumbwa na mafuriko hayo ikiwemo Kichangani, Mjimpya, Mazimbu, Chamwino, Lukobe na Mkundi huku ikiadhiri kaya 233 zenye idadi ya watu 1214 wakiadhirika na mafuriko.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi alieleza kuwa mvua zilizonyesha kati ya mwezi April hadi Mei 2014 yamesababisha mafuriko na kuleta hasara mbalimbali ikiwemo kuharibu miundombinu ya barabara kubomoa baadhi ya nyumba kati ya nyumba 509 na kufanya watu 1214 kuadhirika na maji ya mvua za masika.

Alifafanua kaya zilizokumbwa na maji ya mafuriko hayo kuwa ni Kichangani ambapo kaya 276 ndizo zilizokumbwa zenye wakazi 584 wakati Mazimbu ikiwa na kaya 505 na wakazi 64, Lukobe yenyewe ina wakazi 283 kutoka kaya 6, Chamwino kata 58 na wakazi 221, Mjimpya watu 117 na kaya 45 na Mkundi ikiwa na kaya tano na watu tisa.alisem Amanzi.

Uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mito yanayoingiza maji mto Morogoro ndiyo chanzo cha mto huo kujaa mchangana kuufanya mto kuwa na kina kidogo kinachosababisha maji kushindwa kufuata mto.CHANZO MTANDA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment