Haki za Mwalimu pinda anapoajiriwa na serikali.
WAJIBU MKUU WA MWALIMU
Wajibu mkuu wa mwalimu ambao
ndio Nguzo Tano za kazi ya ualimu
ni:-
1.KWA MTOTO
2.KWA JUMUIYA
3.KWA KAZI YAKE
4.KWA TAIFA
1.KWA MTOTO
Nguzo hii inamtaka mwalimu akubali
kwamba wajibu wake mkuu ni kwa
mtoto ambaye
amekabidhiwa
kumleana kwamba kwa wakati wote
anatakiwa kumwongoza kwa
kumkuza na kumwendeleza
kimwili,kiakili na kiroho.
2KWA JUMUIYA
nguzo hii inamtaka mwalimu kuijua
jumu7iya ambamo anaishi
na kufanyia kazi na kutii mamlaka
halali na tabia yake mwenyewe
kuwas mfano bora kwa
wanajumuiya.
3 KWA MWAJIRI WAKE
Nguzo hii inamtaka mwalimu
kumtumikia mwajiri wake kwa utii na
kwa uaminifu kwa mujibu wa
masharti ya kazi ya ualimu
4.KWA KAZI YAKE YA UALIMU
Nguzo hii inamtaka Mwalimu kufuata
kwa wakati wote na kwahali ya juu
kabisa Maadili mema ya
kazi ya ualimupamoja na:-
kufanya kazi kwa bidii na kwa
kufuata utaratibu
Kuwa mfano mzuri katika tabia
wakati wote kwa watoto waliochini ya
ulinzi wake na hata
watoto wengine katika jamii.
/kujaribu kila wakati kuinua kiwango
cha utendaji nauwezo wa kufanya
kazi
/kutotumia vibaya haki
zinazoambatana na utumishi wa
umma.
5.KWA TAIFA LAKE
Nguzo hii inamtaka mwalimu kuwa
mzalendo na raia mwema na mtii wa
sheria za nchi na mwelekezaji
wa watoto kuwa wazalendo safi na
raia wema wa baadae kwa kuzingatia
wajibu wa mwalimu kwa
kazi yake ya ualimu
Mwalimu anategemewa kuwa na
tabia na mwenendo mzuri wa kufaa
kuigwa na kustahili kupewa
heshima na kuaminiwa na
jumuia,wazazina wanafunzi.
Mwalimu yeyoteanayekwenda
kinyume na maadili na masharti ya
kazi ya ualimu anakuwa nimtovu wa
nidhamu.
HAKI ZA MWALIMU
LIKIZO YA MWAKA(Annual leave)
Kwa mujibu wa kanuni za kudumu za
watumishi wa umma 2009 kifungu
H.5(ii)kikisomwa pamoja na
kanuni za utumishi wa umma,2003
kifungu cha97(i)mtumishi wa umma
anayostahili yaya kupewa
likizo siku 28kila mwaka.Aidha
kifungu cha 97 (ii) kinaeleza kuwa
likizo ni haki ya mtumishi.
Inapokuwa haitolewina mwajiri
kwasababu mbalimbali basi mwajiri
atawajibika kumlipa mtumishi
mshahara wake wa mwezi.Mtumishi
hatopewa likizo ya mwaka hadi
amefikisha miezi 8 tangu
kuajiliwa rasmi(kanuni Na.97:za
2003).Mtumishi atapewa usafiri wa
likizo mara moja ndani ya
mzunguko wa miaka miwili yeye,
mkewe na watoto wane chini ya umri
wa miaka 18 au
wategemezi,kanuni Na.97(5).
LIKIZO YA UZAZI(Maternity leave).
Kifungu Na.98(1),2003 Mtumishi wa
kike atapewa likizo ya uzazi siku 84
mara moja kila baada ya
miaka (3) kumaliza likizo
yake,akijifungua mapacha atastahili
likizo yasiku 100,kwa kwa mujibu wa
T.S.S,2008,47(1)
Kifungu 98 (2 ) Mtumishi
anapojifungua kwa bahati mbaya
mtoto akafariki kabla ya miezi 12
Kumalizika.Akipata mimba atastahili
likizo ya uzazi siku 84.
Kifungua Na. 98 (3). Mtumishi
aliyejifungua astastahili muda wa saa
mbili kwenda
kunyonyesha hadi kipindi cha miezi
sita (6).
Mtumishi wa Kiume, mkewe
akijifungua atapewa likizo ya siku
tatu.
(T.S.S 48)
LIKIZO BILA MALIPO.
Kifungu Na.99 (1) cha kanuni za
utumishi wa umma 2003.Katibu Mkuu
ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma
anaweza kutoa likizo bila malipo
kama ataridhika na
sababu za maombi ya likizo
hiyo.Hata hivyo maombi hayo ni
lazima yapitie kwa Mwajiri
kanuni 99(2).
LIKIZO YA UGONJWA.
Kifungu Na.100 (1) cha ushauri wa
Daktari,Mamlaka ya ajira inaweza
kutoa likizo ya
ugonjwa.Likizo hutolewa miezi sita
na mshahara kamili na miezi sita
mingine kwa nusu
mshahara.
SABATICAL LEAVE.
Kifungu 101 (1) Likizo hii hutolewa
kwa mwajiri ili kukamilisha au
kuimarisha uzoefu.Likizo
hii ni lazima iindhinishwe nakatibu
Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa
Umma.Likizo hii
hupewa Mtumishi si zaidi ya miezi 12
na hutolewa baada ya Mtumishi
kufanya kazi mfululizo
miaka mitano,Kanuni Na.101 (4).
LIKIZO YA KUSTAAFU.(Leave
pending retirement)
Kanuni Na 102 za 2003,Mtumishi wa
Umma atastahili kuomba likizo ya
kujiandaa kustaafu
mwezi mmoja kabla ya tarehe rasmi
ya kustaafu kwake.Atastahili kupewa
usafiri wa
kumrejesha kwao yeye na familia
yake pamoja na mizigo sio chini ya
tani tatu kulingana na
daraja lake.
MATIBABU KWA WATUMISHI WA
UMMA
Kifungu .K.(i) za kanuni za kudumu
2009 ikisomwa pamoja na kifungu
cha
105 cha kanuni za Utumishi wa
umma Mtumishi anastahili kupata
matibabu bure.
Hata hivyo kuna utaratibu wa bima
ya afya.
Mtumishi akilazimika kusafiri
kwenda Hospitali ya Rufaa mwajiri
atahusika
kugharamia posho ya kujikimu na
nauli.
Vitu muhimu.
Barua ya rufaa.
Barua ya ruhusa tota kwa
mwajir
Fomu Appendix K 28$29 Fomu
bya madai ya posho.
Fomu Appendex K/V ya madai
ya naului ikiambatana na tiketi K.26
Kadi ya mahudhurio hospitali
Sickshhet.
FIDIA YA KUUMIA KAZINI.
Kanuni Na.111(1-5) inaeleza hatua
mbalimbali za kufuata pindi mtumishi
anapopatwa na matatizo kazini.
Mtumishi anayeumia atalipwa fidia
sio chini ya shilingin 1,000,000/= na
sio zaidi
zaidi ya shilingi 10,000,000/=
hutemea na hali ya maumivu au
kufariki.
Kifungu ch 110 kinaelezea kwamba
mtumishi anapoumia wakati wa
kuteke laza majukumu ya ajira
yake anastahili fidia na inamtaka
mtumishi
kujikinga na hali ambayo inaweza
kuathiri afya yake.
KUJIENDELEZA
Kanuni Na .103 inaeleza kamba ni
wajibu wa mwajiri kuwaendeleza
watumishi wake.
Kutokana na tathimini ya kazi ,
mwajiri atabainisha mahitaji ya
kuendeleza watumishi.
Watumishi ni lazima wajiendeleze
katika fani kwa lengo la
kuboresha ufanisi.
Kuandaa mpango kazi wa mafunzo
ka watumishi.
-Vtendo vyovote vinavyopingana na
utaratibu za kiutumishi
-Uzembe unaomgharimu mwajiri
-kuiuka maadili ya kazi ya ualimu(ya
utumishi wa umma)
Adhabu zake
-kufukuzwa kazi bila Utumishi.
-kufukuzwa kazi na utumishi
-kushushwa cheo.
-kushushwa mshahara si chini
ya kiwango ulichoanzia kazi
-kulipa gharama au sehemu ya
gharama kwa upotevu au uharibifu
uliotokana na uzembe
-karipio
-Onyo
-Kusimamishwa nyongeza ya
mshahara.
KUTENDELEA NA
MAJUKUMU KA KUPUMNZISHWA
Mtumishi anapumzishwa bila
kusimamishwa kazi na bila kuathiri
maslahi yake..Lengo lake ni kuzuia
kosa lisiendelee kutendeka wakati
wa uchunguzi wa awali ukifanyika,
(kanuni Na.37)
KUSIMAMISHWA KAZI
Mtumishi husimamishwa kazi na
kupewa Hati ya mashtaka.Hatua hii ni
baada ya Mamlaka ya nidhamu
kuridhika kuwa kuna tuhuma za
ukweli dhidi ya mtumishi husika.
(kanuni 38)
KUREKEBISHA MASHTAKA
Mamlaka ya nidhamu inaruhusiwa
kurekebisha mashtaka yasiyo sahii
ndani ya siku zisizozidi 30
tangu Mshtakiwa alipopewa
mashtaka ya awali(kanuni ya 38(3) )
NUSU MSHAHARA.
Mtumishi aliyesimamishwa kazi
anastahili nusu mshahara wake wa
mwezi tu kwa kipindi chote
alichosimamishwa kazi.Iwapo
mtumishi husika hatapatikanana hatia
na hivyo kutofukuzwa kazi au
kutopewa adhabu yoyote atalipwa
nusu mshahara wake ambao
hakulipwa wakati aliposimamishwa
kazi lakini ameadhibiwa kwa adhabu
nyingine, atalipwa robo ya mshahara
wake.
(kanuni ya 38-2,5 na 6.)
KUONDOKA KITUONI MTUMISHI
ALIYESIMAMISHWA KAZI.
Mtumishi aliye simamishwa kazi
haruhusiwi kuondoka kituoni bila
kuruhusiwa kwa maandisghi
na mamlaka yake ya nidhamu
kanuna ya 38 (7)
ATHARI ZA KUFUKUZWA KAZI
Mtumishi akifukuzwa kazi hupoteza
haki zake. Hata hivyo mtumishi
husika atalipwa
pensheni ya mkupuo iwapo wakati
huo alistahili pensheni ya kila
mwezi.Aidha,
mtumishi aliyetiwa hatiani kwa
makosa ya jinai yanayo husu rushwa
au
hujuma,atapoteza haki au madai yake
yote.(Kanuni ya 40.2003)
MTUMISHI ANAPOKABILIWA NA
KESI YA JINAI.
Mtumishi husika atasimamishwa kazi
hadi kesi husika
itakapohitimishwa.Hatua
zakinidhamu hazitachukuliwa au
kuendelezwa dhidi yake.Mashartina
maelekezo yote
yako kwenye kanuni ya 50 na 51
RUFAA
Mtuhumiwa atapewa haki yake ya
kukata rufaa kwenye
MAMLAKA
SAHIHI na MUDA
MUAFAKA. Rufaa kwa walimu
imeelezwa kwenye kanuni Na 126 (1
hadi 3) ya kanuni za
mtumishi wa umma,2003.
Muda wa kuwasilisha rufaa ni siku 45
tangu tarehe aliyopata uamuzi w\a
awali na rufaa ni
lazima iwe kwa maandishi na
inayowekwa wazi sababu za kupinga
uamuzi na adhabu.Mrufani
anapaswa kuipatia mamlaka yake ya
nidhamu nakala ya rufaa.Iwapo
hakufanya hivyo mamlaka
ya nidhamu inapaswa kuwasilisha
taarifa ya mwenendo wa hatua za
nidhamu na
maelezo/utetezi wake dhidi ya
sababu za rufaa ndani ya siku 14,
nakala kwa Mrufani (kanuni
61)
KUAJIRIWA UPYA KATIKA
UTUMISHI WA UMMA
Walimu wanaruhusiwa kuajiriwa upya
katika utumishi wa umma baada ya
kutumikia adhabu
kwa muda usiopunngua miezi
12.Kanuni Na.120(d) ya kanuni za
utumishi wa Umma 2003
imeelekeza kuwa kamati ya mkoa
inatoa uamuzi juu ya suala hilo .
Uamuzi wa kamati ya
mkoa utawasilishawa kwa katibu wa
tume kwa ajili ya kuwaombea kibali
cha kuajiriwa upya
walimu hao kwa katibu Mkuu
kiongozi.
HITIMISHO
Lengo la mada hizi ni kuwaelimisha
na kuwajengea uwezo Waratibu Elimu
Kata , Walimu
wakuu wa shule /Wakuu wa wa
shule na Walimu walimu wote kwa
ujumla katika kutekeleza
majukumu mbalimbali katika maeneo
yenu ya kazi kwa kuzingatia
sheria ,kanuni,taratibu na
miongozo mbalimbali inayotolewa na
serikali katika kuboresha Utumishi
wa umma, mara kwa
mara.
POSHO YA KUJIKIMU
Kanunui ya 13 inaeleza kwamba
Mtumishi wa Umma aliye ajiliwa
anastahili kupewa:-
Nauli yeye na mkewe?
mumewe,watoto na wategemezi
wasiozidi 4
Posho ya kujikimu kwa kiwango na
idadi ya siku itakapokuwa
imeandaliwa na Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais menejiment ya
Utumishi wa Umma.
KUTHIBITISHWA KAZINI.
Kanuni Na.14 za 2003,Mtumishi wa
Umma aliye ajiliwa kwa mashariti ya
kudumu atakuwa
chini ya matazamio kwa kuzingatia
muundo wa Utumishi wake na
haitazidi miezi kumi na
miwili.
Mkuu wa kituo/kazi atawajibika
kutoa taarifa kwa mamlaka husika
kuhusu:-
Mtumishi kuthibitishwa kazini.
Mtumishi kuongezewa muda wa
matazamio ili kumwezesha kufanya
kazi kwa ufanisi.
Utumishi wa Mtumishi kusitishwa.
KUPANDISHWA CHEO(KANUNI
NA.15)
Kupandishwa cheo kwa Mtumishi wa
Umma kutategemea muda wa
uutendaji,utendaji wa kazi
uliokidhi malengo(ufanisi wa kazi) na
Taaluma ya Mtumishi.
Mtumishi akipandishwa cheo
atakuwa kwenye matazamio kwa
muda wa miezi 6.Kanuni
Na.16(1).
UHAMISHO.
Mtumishi anapohamishwa hustahili
mambo yafuatayo;-
Posho ya usumbufu asilimia 10 ya
mshahara wa mwaka(Kanuni za
kudumu za 2009L13 1-
2).
Posho ya kujikimu atalipwa atalipwa
siku 14 akiwa na mweza wake na
watoto wake 4
chini ya umri wa miaka 18 na
wategemezi 2 kanuni za kudumu
2009L(1-2).
Usafiri wake na familia yake pamoja
na mizigo isio chini ya Tani tatu
kutegemea na daraja
lake9kanuni za kudumu za 2010 J1).
UHAMISHO WA KUOMBA.
Mtumishi wa umma hatalipwa
chochote anapoamba uhamisho kwa
manufaa yake (isipokuwa
)kama amekaakituo kimoja sio chini
ya miaka mitano mfululizo au kama
anataka kwenda kwao
kujianda na kustaafu na awe
amefanya kazi nje ya mkoa wake si
chini ya miaka 10
mfululizo.(L.8 a-b)
KUSTAAFU.
1.Kustaafu kwa hiari.
Itakuwa miaka hamsini na tan,
.Sharti atoe taarifa ya kusudio lake
miezi sita kabla ya kutimiza miaka
55
2 Kustaafu kwa ugonjwa.
Kanuni namba 30,2003
Sheria namba 2 ya pensheni ya
itimisho la kazi.
Kwa ushauri wa daktari na jopo la
madaktari mamlaka inaweza
kupendekeza mwalimu astaafu
kwa ugonjwa.
3Kustaafu kwa lazima.
Mtumishi wa umma atalazimika
kustaafu kwa lazima atimizapo umri
wa miaka sitini.
Atawajibika kutoa taarifa miezi sita
kabla ili aweze kupata kibali kwa
wakati .
MAFAO YA KUSTAAFU.
PENSHENI
MIRATHI
KIINUA MGONGO cha mkataba wa
muda maalum.
PENSHENI.
Pensheni ni mafao ya hitimisho la
kazi kwa mtumishi anaye staafu
kwa:-
lazima. Miaka 60.
kwa hiari. Miaka 55.
kwa ugonjwa
Pensheni inayolipwa na hazina ni
kabla ya 1.7.2004, hii ni kwa mujibu
wa kifungu cha 73 (2)
cha sheria ya mafao ya hitimisho la
kazi na 2 ya 1999 NIDHAMU
AINA ZA MAKOSA NA ADHABU
ZAKE.
Sera ya menejimenti na ajira katika
utumishi wa umma ya mwaka 1999
katika aya za 5.37-37
zimeeleza kuwa KOSA ni kitendo cha
utovu wa nidhamu kutokana na
kukiuka maadili, kanuni
na masharti ya kazi.
Utaratibu wa kuzingatiwa katika
kushughulikia utovu wa nidhamu
umeelezwa bayana na
kwamba adhabu zitatolewa kulingana
na uzito wa kosa.
Kwa mujibu wa kanuni Na.42 (2) na
43 (2) za kanuni za utumishi wa
Umma za mwaka
2003,aina za makosa na adhabu zake
zimeainishwa katika nyongeza Na.2.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI
WA KUCHUKUA HATUA ZA
NIDHAMU.
(a) uchunguzi wa awali. Kanuni
Na.36
ni lazima mamlaka ya nidhamu ifanye
uchunguzi wa awali kabla haijaanza
hatua za nidhamun
dhidi ya mtumishi. Hatua hii inasaidia
kugundua ukweli kuhusu ukiukwaji na
kujiridhisha
kuwa mtumishi amehusika na kuwa
kuna uwezekano wa kuthibitisha
kosa dhidi yake. Hatua
hii inapunguza uonevu unaoweza
kuwepo kwa uchukuaji wa hatua za
nidhamu kwa pupa.
(b) makosa na adhabu,kanuni Na.53
na 59.
makosa madogo madogo (summary
proceedings) kanuni Na. 43.
-kuchelewa kufika kazini
-kutokuwepo kazini muda wa kazi
-kutokamilisha kazi.
-uzembe katika kutekeleza
majukumu.
-kutotimiza maelekezo ya utendaji
kazi.
mara ya kwanza – barua ya onyo
mara ya pili – karipio
mara ya tatu – kusimamisha
nyongeza ya mshahara.
(c)makosa makubwa (formal
proceedings) kanuni Na.42
-kutofika kazini zaidi ya siku 5
-vitendo vinavyo husu wizi,rushwa
-uzembe uliokithirikatika kutekeleza
majukumu
-kujihusisha na kazi nyingine nje ya
ofisi saa za kazi.
VITU VYA KUANDAA UNAPOJAZA
1.MKATABA WA AJIRA
FOMU ZA MKATABA NAKALA 3
PICHA ZA UTUMISHI
CHETI CHA TAALUMA(UALIMU)
NAKALA 3
CHETI CHA FORM FOUR/SIX
NAKALA 3
2.USAJILI PENSHENI
1.BARUA YA AJIRA (YENYE TSD
NAMBA)
2.BARUA YA KUTHIBITISHWA
KAZINI
3.SALARY SLIP HALISI
4.PICHA 2
3.KUSTAAFU
1. BARU A YA AJI RA ( YENYE T SD
NO)
2. BARUA YA KUTHIBITISHWA
KAZINI
3. BARUA YA KUPANDA CHEO CHA
MWISHO
4. SALARY SLIP
5. PICHA TATU
6. KIBALI CHA KUSTAAFU (ukipate
TSD Wilaya)
7. UJAZE FOMU ZA PSPF NO 6.
4.KUANDAA MIRATHI-MAHITAJI
1.MUHTASARI WA
WANANDUGU KUMCHAGUA
MSIMAMIZI WA MIRATHI
2.HAKI YA USIMAMIZI WA
MIRATHI(HALISI)
3.CHETI CHA KIFO(HALISI)
4.BARUA YA AJIRA
(YENYETSD) NAKALA
5.BARUA YA
KUTHIBITISHWA KAZINI
(NAKALA)
6.BARUA YA KUPANDA
CHEO CHA MWISHO
(NAKALA)
7.SALARY SLIP-(HALISI)
8.CHETI CHA NDOA/ KIAPO
CHA NDOA-(NAKALA)
9.KIAPO CHA MJANE/
MGANE KUTUNZA WATOTO
10.VYETI VYA KUZALIWA
WATOTO/KIAPO(CHINI
MIAKA 21)
11.BARUA TOKA SHULENI
KUTHIBITISHA KAMA
MTOTO ANASOMA
12.PICHA 8 ZAMSIMAMIZI
WA MIRATHI
13. PICHA 3 ZA KILA MTOTO
WA MAREHEMU
14. PICHA 3 ZA MJANE/
MGANE
15.KADI ZA BENKI ZA
WALIOPO KWENYE MGAO
(NAKALA)
16.FOMU NA VI YA MGAWO
WA MIRATHI(ofisini
utapewa)
17.FOMU NA8 NA 9 ZA
PSPF (ofisini utapewa)
VYOTE LAZIMA VIPITIE
MAHAKAMANI NA MHURI NA SAINI
YA HAKIMU
KILA MTU AVIANDAE AU ATUNZE
KUMBUKUMBU ZA UTUMISHI
KWA SABABU NI TOKIO LA KILA
MTU
0 comments :
Post a Comment