-->

MWILI WA MAREHEMU MAMA YAKE ZITTO KABWE WASAFIRISHWA KWENDA KIGOMA

 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwilki za Saida Salum, mama mzazi wa Zitto, Jumapili Juni 1, 2014.


Mama yake Zitto, alifariki mapema saa 5 asubuhi, akiwa na umri wa miaka 64, kwenye hospitali ya AMI, Msasani jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya kizazi. Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cah Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri). Ameacha mume, na watoto 10, wanaume 6 na wakike wanne. alisema Zitto.


Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment