-->

WASHIKIWA WA MAUAJI YA MPEKETONI WAUAWA NCHINI KENYA


Serikali ya Kenya inasema kuwa washukiwa watano wa mauaji ya watu 50 mjini Mpeketoni Pwani mwa Kenya wameuawa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya usalama kuhusu mauaji hayo yaliyofanyika Jumapili usiku na Jumatatu
Katika taarifa hiyo iliyotolewa kupitia kwa mtandao wa Twitter, waziri alisema washukiwa watano waliuawa wakitoroka ikiongeza kuwa bunduki tatu aina ya AK-47 zilinaswa
Taarifa hiyo pia inasema kuwa silaha nyinginezo zilinaswa.
Kumekuwa na malumbano miongoni mwa wanasiasa nchini Kenya kuhusu aliyetekeleza mashambulizi hayo
Afisaa mmoja mkuu katika jimbo la Lamu, alithibitisha kwamba jeshi la Kenya lilipelekwa katika eneo hilo kufuatia mashambulizi ya Jumapili, katika eneo la Mpeketoni ambapo takriban watu 50 waliuawa katika shambulizi la kwanza.
Shambulizi la pili lilifanyika Jumatatu katika kijiji jirani ambpo watu wengine 9 waliuawa.
Kundi la wapiganaji la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ingawa serikali ya Kenya ilisema kuwa yalichochewa kisiasa. Rais Kenyatta aliwalaumu wanasiasa kwa kuwachochea wananachi pamoja na makundi ya wahalifu kutumia nafasi ya utovu wa usalama kufanya uhalifu.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment