HUKU
watu karibia 60 nchini kenya wakiuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi,
katika hali isiyo ya kawaida nchini Tanzania, walinzi wa Maduka ya
Mlimani City jijini Dar wamejikuta wakipata mchecheto wa aina yake baada
ya kitu kilichodhaniwa ni bomu kukutwa kwenye eneo la kuegeshea
magari.
Walinzi wa maduka ya Mlimani City jijini Dar wakikagua kitu kinachosadikika kuwa ni bomu.Tukio
hilo lilitokea Juni 16, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa shuhuda
aliyeomba kusitiriwa jina, aliona gari dogo jeupe likiangusha kifaa
hicho kilichodhaniwa ni bomu kisha likatoweka.
Chanzo
hicho kilizidi kudai kuwa baada ya gari kutoweka, dada mmoja alipita
eneo hilo na kukuta kitu hicho kilichofungwa nyaya kikiwa ndani ya
mfuko, akashtuka na kwenda kumtonya mlinzi wa eneo hilo ambaye alifika
mara moja na kuwaita wenzake.
Taarifa
za uwepo wa kifaa hicho ziliwafikia waandishi wetu waliokuwa wakipiga
doria katika eneo hilo na haraka wakasogea karibu kuwashuhudia walinzi
hao wa Kampuni ya Ulinzi ya Omega wakiwa wamekizunguka kifaa hicho kwa
umakini mkubwa.
Walinzi hao
walimuita kiongozi wao ambaye alifika na kukichunguza kifaa hicho ambapo
alipokifungua aligundua ni betri bovu la pikipiki.Waliichukua betri
hiyo na kuitupa huku wakitawanyika kurudi kwenye maeneo yao ya ulinzi.
Eneo la Mlimani City.
0 comments :
Post a Comment