Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo
MTOTO
Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria
wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili
kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Akizungumza
kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa
Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama
yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia
kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
Anasema
tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa
matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na
kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.
Anasema
tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza
kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda
iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute
Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.
Ameongeza
kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka
Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda
kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao
hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza
kutatuliwa tatizo lake.
Aidha
kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa
wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na
kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za
matibabu kuwa kubwa.
Amesema
anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri
kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo
Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.
Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.
|
0 comments :
Post a Comment