-->

MAHAKAMA KUU YA RUFAA YAAMURU GOOGLE KUFUTA VIDEO INAYOMKASHIFU MTUME MUHAMMAD(S.A.W)


Mahakama kuu ya Rufaa nchini Marekani juzi imeiamuru Google Inc kuondoa picha za video za filamu ya 'Innocence of Muslims' katika mtandao wake wa Youtube.

Filamu hiyo ilisababisha maandamano makubwa duniani na kuuawa kwa watu wanne pamoja na balozi wa Marekani nchini Libya katika mji wa Benghazi.

Filamu ya 'Innocence of Muslims' iliyotengenezwa Nakoula Basseley Nakoula maudhui yake yalikuwa ni kupotosha ukweli wa dini ya kiislamu na kumchamfua Mtume Muhammad ï·º

Mwanzoni Google ilikataa kuondoa filamu hiyo kutoka YouTube, pamoja na shinikizo kutoka White House pamoja na mashirika na jumuiya mbalimbali kote dunia zilizosema kuwa filamu hiyo inachochea chuki za kidini. Trailer ya filamu hiyo imefungiwa nchini Misri, Libya na baadhi ya nchi nyingine.

Mahakama ya Rufaa ya Marekani Imekataa utetezi wa Google ambayo imedai kuwa kufutwa filamu hiyo katika ukurasa wa Youtube kunakiuka uhuru wa kusema.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment