Nyoka huyo alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla. Tukio
hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na
kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili. Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini. Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.

Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji
Chatu ameshinda vita
vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba,
kumpinda na kisha kumla. Tukio hilo
lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera
na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.Nyoka huyo mwenye
urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo
alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBFYA HAPA CHINI

Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi
Tiffany Corlis,mkazi
wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo
la ajabu sana, '' aliambia BBC "tulimuona Nyoka
akipambana na Mamba , alifanikiwa kumpinda mamba na kumzunguza hasa katika
sehemu ya miguu ya ili kumdhibiti.'' "pambano
lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya
maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.'' "baada ya Mamba
kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kunza kumla,'' alisema
Tifanny.
Baada
ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Bwana Corlis alisema
kuwa ilimchukua Nyoka dakika kumi na tano kuma yule Mamba.
''Bila shaka Nyoka
huyo alishiba vyema, na hatuui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama
huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena. Mtu mwingine
aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili
walipambana kwa karibu masaa 5. Hatimaye wote walionekana kuchoka. ''Sio kitu unachoweza
kuona kila siku,'' alisema Alyce.
CHANZO: BBC SWAHILI


0 comments :
Post a Comment