Mwakilishi
wa wachezaji wa Barcelona, Patrick Kluivert alisema jana mechi hiyo itawahusisha
wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davis,Gaiza Mandieta, Ludovi Giuly,
Francesco Coco na wengine waliopita kwenye timu hiyo.
Kluivert alisema "ameshakuwa mwenyeji hapa
Tanzania kwani ni ujio wake wa tatu na anaamini kuwa mashabiki wanapenda sana
mpira wa miguu , itakuwa fursa kubwa kwao kuviona vipaji vya zamani ambavyo
vimetukuka, hivyo amewataka mashabiki waje uwanja wa taifa kuona mpira wenye
ushindani," alisema Kluivert.
Mwakilishi wa kampuni ya
PrimeTime Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu hiyo Barcelona, Stuart
Kambona alisema kuwa madhumuni ya mchezo huo ni kudumisha mahusiano ya
kibiashara ya mpira wa miguu kati ya Tanzania na Hispania, pia kuitangaza
Tanzania kwenye sekta ya utalii.
0 comments :
Post a Comment