Kwa mujibu wa televisheni ya ntv ya Kenya.
Mheshimiwa ameuawa pamoja na dereva wake pamoja na walinzi wake wawili
majira ya saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo katkka barabara ya
Kenyatta avenue wakati akiwa njiani kutoka katika sherehe.
Alisimama na ili kununua magazeti,na ndipo mtu aliyevalia mask
alipojitokeza kutoka gari ndogo aina ya toyota pro-box na kuanza
kuwafyatulia risasi vichwani kila mmoja,akitumia bunduki aina ya AK 47.
Pia alipora briefcase ya marehemu pamoja na bastola mbili za walinzi
wake na kutokomea kusikojulikana akitumia gari hilo lililokuwa
limefichwa namba zake.
Marehemu pia alikuwa ameambatana na mke na watoto wake wawili wa kike
waliokuwa ndani ya gari la nyuma na walishuhudia mauaji hayo
yakifanyika.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Kenyatta hospital Nairobi.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment