-->

CHAMA CHA ALBINO KUMSHITAKI RAISI KIKWETE UMOJA WA MATAIFA

Msemaji wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Josephat Torner
 Msemaji wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Josephat Torner
CHAMA cha Albino Tanzania (TAS), kimetoa miezi mitatu kwa Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati vitendo vya mauaji ya albino yanayoendelea nchini. Akishindwa kuchukua hatua, watamshitaki Umoja wa Mataifa (UN). Anaripoti Sarafina Lidwino … (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Online, Afisa Habari wa TAS, Josephat Torner amesema, wamechoshwa na vitendo vya mauaji ya albino vinavyoendelea huku Rais Kikwete akiwa kimya.
Torner amesema Rais Kikwete ni rais wa Watanzania wote hivyo analazimika kukomesha mauaji ya albino na akishindwa kuchukua hatua katika kipindi hicho walichompa watapeleka malalamiko yao UN.
Alisema watalazimika kufika huko kwani chama chao kimesajiliwa chini ya UN hivyo wakishindwa kusaidia wa Rais Kikwete watalazimika kukimbilia huko ambako wana imani watasaidiwa.
Msemaji huyo alisema kabla ya kupeleka malalamiko yao UN watafanya maandamano makubwa Machi 2, 2015 nchini nzima, na kwa upande wa Dar es Salaam wataanzia Ocean Road na kumalizikia Ikulu ambapo wamepanga kumuona Rais Kikwete na kumpa malalamiko yao.
“Maandamano hayo ya amani yatakuwa na kauli mbiu ‘MAUAJI YA ALBINO SASA BASI’. Mikoani Albino wataandamana kwenda ofisi za wakuu wa mikoa kupeleka vilio vyao,” alisema Torner.
Tangu mwaka 2006 zaidi ya Albino 76 wameuawa, na majeruhi waliopo ni zaidi ya 56 na makaburi 18 yamefukuliwa na kuchukuliwa miili ya waliozikwa huku walioachwa na ulemavu wa kudumu ni 11, hakuna muuaji hata mmoja aliyekamatwa.
SOURCE:MWANAHALISIONLINE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment