Licha ya madai yanayotolewa na serikali ya Marekani juu ya kukabiliana
na ubaguzi nchini humo, siku chache tu tangu yalipotokea mauaji ya
wanafunzi watatu Waislamu mjini Chapel Hill, Waislamu wengine wawili
wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na mtu mmoja mwenye chuki dhidi
ya Uislamu.
Habari zinaeleza kuwa, mtu huyo mkazi wa mji wa Detroit katika jimbo la
Michigan, aliwashambulia na kuwajeruhi vibaya kwa kisu Waislamu hao
wawili kwa lengo la kuwaua.
Duru za habari kutoka mjini Detroit zimefafanua kuwa, shambulizi hilo
dhidi ya Waislamu hao, lilijiri katika kituo cha basi huku watu
wakiangalia.
Vyombo vya habari vimemtaja mshambuliaji kwa jina la Terrence Lavaron
Thomas mwenye umri wa miaka 39. Inaelezwa kuwa, baada ya Terrence
kuwashambulia Waislamu hao ambao wana umri kati ya miaka 52 na 51 wote
wanaume, alitiwa mbaroni na polisi ya mji huo akiwa mitaani.
Mashuhuda wameeleza kuwa shambulizi hilo, lilitekelezwa kwa sababu ya
chuki za kidini, huku vyombo vya habari vikijaribu kupotosha ukweli wa
tukio hilo, na kudai kuwa, mshambuliaji huyo alikuwa ametumia madawa ya
kulevya na wala hakufanya shambulio hilo kwa msingi wa chuki dhidi ya
Uislamu.
Hili ni shambulizi la pili kujiri ndani ya kipindi cha siku 10 tu, baada
ya tukio la mauaji ya Waislamu watatu katika mji wa Chapel Hill katika
jimbo la Carolina Kaskazini.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
0 comments :
Post a Comment