Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na
Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia
kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International
Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya
katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na
maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo
wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Kutoka
kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais
wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho
Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni
(Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa
mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika
Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya
kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20,
2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi. Picha na IKULU
Tanzania
inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na muumini mkubwa wa
Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jijini Nairobi mara baada ya
kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye
amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
"Tunaamini
kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua
nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na
dunia kwa ujumla" Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa
masoko yaliyogawanyika, miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi
katika dunia ya leo wala ya baadaye.
Rais
Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji
wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha
uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha wana Afrika Mashariki
katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya kuendeleza Jumuiya ambayo
inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Rais
Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara
imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona
matunda hayo. Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika
nchi za EAC imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola
5,805.6 ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la
asilimia 6.
"Kama
biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika, ongezeko hili la
biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia wakati muafaka
kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano wetu" Rais amesema
na kuongeza kuwa " kwa njia hii serikali zitakusanya kodi na hivyo kuna
umuhimu wa kuelekeza nguvu katika kusaidia biashara ndogo ndogo na zile
zisizo rasmi kwa kuziwekea mazingira mazuri".
Rais
Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa
na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan
Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki
ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata
uanachama katika EAC yanaendelea.
0 comments :
Post a Comment