-->

ULIMBOKA AFUNIKA LIGI DARAJA LA KWANZA,WATU WAJIULIZA KWA NINI ALIACHWA SIMBA

Uli akitafuta mbinu za kufunga bao


Uli akishangilia bao la pili zidi ya Wanajeshi wa Rhino Rangers ya Tabora








Uli Kulia akipongzwa na wenzake







Uli akiparamia boda boda kuelekea Nyumbani kwake Kihonda baada ya kuhojiwa na Mtandao huu.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MCHEZAJI wa zamani wa Simba na timu ya Soka ya Taifa Tanzania‘Taifa Stars’Ulimboka Makingwe’Uli’ a.k.a Mnyambara amepeleka salama klabu yake ya zamani ya Simba baada ya kung’ara katika ligi daraja la Kwanza akiitumia timu ya Burkinafaso ‘Wanakisiki Cha Mpingo’ ya Mkoani hapa.
Uli ametoa tambo hizo baada ya kuonyesha uwezo Mkubwa katika ligi hiyo ambapo katika michezo mitano aliyocheza toka ajiunge na timu hiyo amefanikiwa kufunga magori matano.
Mchezaji huyo aliyewahi pia kuzichezea timu za Reli ya Morogoro na Mtibwa Sugar, amesaini mkataba wa kuitumia timu ya Burkinafaso kwenye michezo ya nyumba pekee kufuatia mchezaji huyo kutingwa na ubize wa biashara zake hivyo kushindwa kusafiri na timu hiyo mikoani, katika michezo mitano ya raundi ya pili ligi daraja la kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Jamhuri Uli alifanikiwa kupachika mabao hayo matano na kuipaisha timu hiyo iliyokuiwa kwenye janga la kushuka daraja.
Ikumbukwe katika mzunguko wa kwanza Burkina haijashinda hata mchezo mmoja huku kitoka sale michezo yote ya nyumbani ambapo raundi ya pili Burkina akiwa na Uli iliicha Polisi Mara bao 4-1 huku Uli akifunga bao 1 na mchezo wa pili Burkina ya Uli ilichapa tena Polisi Dodoma bao 4-0 huku Uli akipiga bao 2 na majuzi Burkina ya Uli ilichapa Rhino Ranger ya Tabora bao 4-0 Uli tena akipiga bao 2.
Akizungumza na Mtandao huu Uli alisema” Kwa sasa niko fiti michezo yote iliyobaki nitafunga mabao zaidi ya mawili kwenye ligi daraja la kwanza hakuna beki wa kunizuia kufunga mabao wewe mwenyewe shahidi mechi 5 nimepiga bao 5 zile mechi mbili za awali za Geita na Toto Afrika sikuwa na mazoezi ya kutosha ndio maana nilishindwa kucheza vizuri hii ni salama kwa Simba inaniuma sana kwa timu yangu ya samba mchezaji anapata nafasi zaidi ya 5 anashindwa kufunga bao hata moja mimi nikipata nafasi 5 napiga bao 2 au tatu”alisema Uli.
SOURCE:SHEKIDELE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment