Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Chanzo: Gazeti la Nipashe, Feb 20, 2015.
0 comments :
Post a Comment