Mtoto wa
kiume wa miaka miwili ni mmoja ya watu walionusurika kufariki katika
ajali ya ndege ya TransAsia iliyoua watu 31 huko Taiwani baada ya kukosa
mwelekeo na kuanguka mtoni katika mji wa Taipei.
Mpaka sasa
tayari watu 15 wameokolewa ikiwemo watoto wengine wanne ambao umri wao
haujatajwa huku watu wengine 12 hawajulikani walipo.
Mtoto huyo alikutwa akilia nje ya ndege hiyo na kuchukuliwa na waokoaji kisha kumkimbiza hospitali.
Ndege hiyo
iliyokuwa na abiria 58 ilipita karibu na magari na kudondoka mtoni muda
mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan, Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijajulikana.
0 comments :
Post a Comment