Katika
sehemu ya kwanza ya makala hayo tuliishi kwa kuona Naibu Meya mstaafu
Lidya Mbiaji akieleza namna ya tabia hatarishi zinachangiwa na wamikili
wa kumbi za sterehe juu ya biashara ya ngono namna ilivyovatikisa
Morogoro sasa tuendelee na habari hiyo......
Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mbiaji alisema kuwa tabia hatarishi zinachangiwa na wamikili wa kumbi za sterehe ambapo machangudoa wamekuwa wakifanya biashara zao za kuuza miili na hali hiyo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nao wamejiingiza huku kundi lingine la wafanyakazi wa ndani na wanawake waliopo ndani ya ndoa wakiwa katika kundi.
Wanawake
walioolewa na wafanyakazi wa ndani hawana vituo maalum vya kuuza ngono
isipokuwa kundi lingine la wanafunzi wa shule za msingi, sekondari,
wenyewe wanaungana na kundi lililoshindikana katika biashara hiyo katika
maeneo maalum katika kumbi za sterehe.
JAMII NA VIONGOZI WANAFUMBIA MACHO.
“Baada
ya utafiti wetu maeneo mbalimbali, tuliwaita wafanyabiashara na
kuwaeleza hali halisi ya maambukizi mapya namna mkoa wa Morogoro
inavyoongezeka kasi kwa wagonjwa wapya lakini hali ni ile ile na wenye
thamana ya kuwafutia leseni wafabiashara kumbi za sterehe wamekaa kimpya
baada ya kuwasilisha ripoti yetu lakini ni kweli kumbi hizo
zinazochangia kufuga machagundoa.”alisema Mbiaji.
Alisema
kuwa achilia mbali kumbi za sterehe kuficha kundi hilo kwa nyakati zote
za mchana na usiku lakini hao wenyewe makahaba, machangudoa, wasenge na
wengine wamekuwa wakiitaka serikali iwatambue ili kuepukana na
unyanyasaji kutoka kwa madaktari pindi wanapoumia kutokana na maumbile
makumbwa sehemu za siri ama haja kubwa.
“Kwanza
wenyewe hao machangudoa na mashoga wanataka serikali itunge sheria za
kuwatambua ili hata hospitalini pindi wanapoenda kutibiwa
wasinyanyapaliwe na madaktari pindi wanapoumizwa wakati wa ngono au
kuingiliwa kimaumbile kwani wamekuwa wakiumia sehemu za haja kubwa na
maumbile makubwa na wamekuwa wakiyasema hayo wakati tunapowaita kuwapa
semina za maambukizi ya ukimwi kwa makundi hayo.”alisema Naibu Meya huyo
mstaafu.
Licha
ya kutaka serikali itungwe sheria za kuwatambua na shughuli zao hizo
lakini wanaitaka serikali inunue vilainishi (mafuta maalumu na kondom
maalum kwa kazi hiyo) ili mashoga na machangudoa wawe wanaitumia ili
kuepusha kuumia wakati wa kutoa huduma kwa wateja wao.
WIKIENDI HUCHUKIWA NA MAKUNDI HAYO.
Mbiaji
aliendelea kufichua siri za mashoga na machangudoa wauza ngono kuwa
siku hizo za jumamosi na jumapili pamoja na siku za sikukuu zimekuwa
shida kwao kutokana na kukosa wateja wa uhakika kutokana na wateja wao
ambao ni wanaume wa watu kutokwenda kazini kukosa mapato ya kutosha.
Manispaa kuchukua hatua ya kubidhiti.
Baada
ya kuyatambua makundi hayo ili kuachana na kazi hiyo, halmashauri ipo
tayari kutoa mikopo ya liba nafuu ili kuwakopesha pesa ili wafanye
biashara halali huku ikiwapigia magoti wamiliki wa kumbi za sterehe
kusaidia kuwashaswishi makundi hayo kuachana na kazi hiyo na kujiingiza
katika biashara za ujasiliamali.
“Wazazi
nao wanapaswa kuwa makini na malezi ya watoto wa jinsia zote hasa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuwadhibiti ili wasizurule
ovyo nyakati za jioni na usiku kwani mwanya huo hutumiwa vizuri na
watoto wenye kuiga tabia za kimaghalibi kutokana na baadhi ya wazazi
kushindwa kutimiza majukumu ya malezi.”alisema.
Mbiaji
alisema kuwa kinachoumiza zaidi ni kusikia wanafunzi wa shule za msingi
wakijiingiza katika biashara hiyo kwani ni kundi ambalo lilikuwa
halijaingia katika vitendo vya uuzaji wa ngono lakini sasa hivi tayari
nao wameingia rasmi kutokana na dada zao wa sekondari kujiingiza.
Tulitoa pendekezo.
Mbiaji
alisema kuwa baada ya kuunda kamati iliyoundwa kufuatia makundi
yaliyovamia Morogoro ilitoa mapendekezo ya kufutiwa leseni za biashara
katika zile kumbi za sterehe zilizokiuka taratibu na sheria za nchi
lakini wenye mamlaka na suala hilo wamekaa kimya na tatizo kuendelea
kukua siku hadi siku.
“Kazi
ya kuyatambua makundi hayo ilifanyika kwa upelelezi wa hali ya juu
kwani ilishirikisha viongozi wanne wa dini ya kiislamu na kikristo,
madiwani watatu, watendaji watatu wa halmashauri nikiongoza jahazi mimi
mwenyewe na watu waliotuona walishindwa kutofautisha kwani wanawake wote
tuvaa nguo fupi na watu walivaa kihuni ili kulingana na uhalisia na
mienendo ya machangudoa huku wanaume katika msafara huo wakifanana na
tabia za mashoga.”.alisema Mbiaji.
Ni
mambo ya aibu yaliyoonekana katika vyumba vya makahaba baada ya
kushuhudia makundi hayo kwa kuwaona wanaume wanne na wanawake wanne
wakiwa chumba kimoja, vitanda viwili wakifanya vyao achilia mbali
waliokuwa wakifanya kazi hiyo kitandani wengine walikuwa wameshika ukuta
lakini ni lazima ulipia fedha mlangoni kiasi cha sh 1,000.
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA MWANZOMGUMU KATA YA MWEMBESONGO.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa Mwanzomgumu kata ya Mwembesongo Mmanispaa ya
Morogoro, Saidi Omari Kamba (66) yeye alisema kuwa biashara ya makahaba
ipo katika eneo lake la mtaa wa Mwanzomgumu sehemu ya Msamvu Itigi na
sasa biashara hiyo inatimiza mwaka wa pili.
Kamba
alisema kuwa tetesi za wanawake hao kufanya biashara ya ngono
zimemfikia katika ofisi yake kutoka kwa wazazi wakilalamikia tabia
zinazofanywa na machangudoa hao kuwa wamekuwa kero hasa kwa maadili
yanatokana na uwepo wao jirani na makazi ya watu ambayo kumetapakaa
watoto wadogo ambao ni rahisi kuiga tabia hiyo.
“Mimi
kama mwenyekiti baada ya kupata taarifa za uwepo wa makahaba nilifanya
uchunguzi na kubaini ukweli na kingine nilichoelezwa kuwa kuna tetesi za
wanawake hao kupangisha moja ya nyumba na kulala kisha giza likianza
kuingia, kujisogeza eneo la Msamvu Itigi na kuanza kuuza miili yao kwa
wanaume kwa lengo la kupata ujira wa fedhaa.”alisema Kamba.
Kamba
alisema kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na kundi kama hilo lakini kundi
hilo lilikuwa limejisitiri katika nyumba maalumu na athari zake zilikuwa
ndogo sana tofauti na sasa hivi ambako wanawake hao wamekuwa wakiuza
miili yao sehemu ya wazi tena hata watoto hawajalala.
“Tumefanya
vikao vingi na wazazi juu ya namna ya kuwaondoa wanawake hao lakini
serikali ya mtaa haina ubavu wa kuwaondoa lakini suala hili tumefikishaa
katika ngazi za juu lakini na wao wamekaa kimya sasa kero imebakia
kupokea malalamiko kila kukicha kutoka kwa wazazi.”alisema Kamba.
MFANYABIASHARA WA KWANZA MSAMVU.
Leonard
Mwofuga yeye ni mfanyabiashara mwanzilishi ambaye alikuwa
mfanyabiashara wa kwanza kuweka kibanda cha biashara mwaka 2000 hadi leo
mwaka 2014 anaeleza historia ya eneo la Msamvu stendi na namna
machangudoa walivyovamia.
Mwofuga
anasema kuwa februari mwaka 2000 ndiye yeye alianza kuweka kibanda cha
biashara baada ya serikali kuhamisha stendi kuu ya mabasi yaendapo
mikoani katikati ya mji na kuhamishia Msamvu ambao sasa panajulikana
kama Msamvu Itigi na jina la Itigi lilitokana na mama lishe wenyeji wa
Itigi kutoka Singida waliomiminika mmoja baada ya mwingine hadi leo eneo
hilo limesheheni wafanyabiashara wa kila aina.
Eneo
la Msamvu stendi kabla ya stendi kuhamishiwa eneo hilo lilivuma kwa
majina ya Msamvu kwa Mela, Msamvu kwa Lupilo, Msamvu Hay Way, Msamvu BP
lakini majina hayo yalipungua nguvu tangu mwaka 2012 baada ya
mfanyabiashara mmoja wa vinywaji kuhamia eneo hilo na kundi la
machangudoa, makahaba, wasenge na mashoga akihama nao kutoka katikati ya
mji na kuhamia eneo hilo ambalo kwa sasa linajulikana kama Msamvu
Itigi.
Neno
Itigi lilivuma kutokana na mama lishe waanzilishi wa kuuza chakula
akiwemo mmoja wao aliyefahamika kwa jina la mama Mbarouku akitokea
katika mji mdogo wa Itigi Singida sambamba na wahudumu wake waliokuwa na
jukumu la kuhudumia wateja wake wa chakula wakitokea katika mji mji huo
mdogo wa Itigi kwa mwaka 2001.
“Nakumbuka
vizuri maana halisi ya jina la Itigi linatokana na akinamama wauza
chakula kutoka mji mdogo wa Itigi mkoani Singida lakini sasa hivi
limebadilika maana yake, kwa sababu sasa hivi Itigi ya Msamvu Morogoro,
tafsiri yake ya haraka ni Itigi inayopatikana machangudoa na siyo Itigi
ile ya mwaka 2000 ilikuwa na maana ya kupata huduma ya kulala bora na
safi kwa wageni mbalimbali wakiwemo wasafiri na madereva.”alisema
Mwofuga.
Zamani
neno Itigi ilivuma kwa nia njema tu tena ikiwa na maana mama lishe na
wafanyakazi wao wakitoka Itigi mkoani Singida lakini sio kwa sasa hivi
neno Itigi linavuma kutokana na kushamili kwa kila aina ya wauza ngono
wa kila rika kuvamiwa hali iliyosababisha usumbufu wa kila aina sio kwa
wafanyabiashara tu bali hata jamii inayoishi jirani na eneo
hilo.aliongeza Mwofuga.
“Kwa
mfano mimi, familia yangu kuanzia watoto wa kike, wavulana na mama yao
hata majirani zangu nimewapiga marufuku kutotembelea eneo la biashara
yangu ama eneo la Msamvu Itigi na hii inatokana na hali halisi kwani
kimsingi sio mzuri kimaadili kutembelewa na mtu anayekuheshimu, acha
mambo haya yaishie kwangu mimi kwa sababu nina saka pesa kama unavyojua
pesa husakwa katika mazingira magumu ikiwemo haya.”alisema Mwofuga.
Eneo
hili lina karaha ya kila aina hasa jua likizama kwani utashuhudia
utitiri wa machangudoa, wasenge, makahaba na mashoga wakianza kutanda na
kujibaza kando ya malori na nguo zao za nusu utupu wakiwasubiri wanaume
kuwachukua na kwenda kufanya nao ngono.alisema mfanyabiashara huyo.
Mfanyabiashara
huyo alisema kuwa karaha inayopatikana eneo hilo ni pamoja na kuzagaa
ovyo mipira ya kiume, kukosa wateja wa kununua bidhaa za wafanyabiashara
maeneo hayo hasa wale viongozi wa serikali na wateja wengi
wanaojiheshimu na kero za hapa na pale kwa baadhi ya wateja wao kuibiwa
mali baada ya kuwekewa madawa ya kulevya katika vinywaji na machangudoa
hao.
“Mwandishi
kama utapata muda wewe njoo eneo hili la Itigi hapa Msamvu saa 4 usiku
utaona mwenyewe kinachofanyika na utakili niliyokueleza yote yana
ukweli mtupu na hapo nyuma kuna vibanda vinavyotumiwa na machangudoa wa
bei ya chini na wale wenye machangudoa wenye kiwango cha juu humpeleka
mteja wao katika vyumba vya kulala wageni katika eneo hilo hilo.”alisema
Mwofuga.
Alisema
kuwa machangudoa hao wameambukiza tabia mbaya kwa wafanyakazi wa
majumbani kuacha kazi na kuingia katika biashara hiyo ikiwa ni muda
mfupi baada ya kuingia kwa mwajili wake wakitokea vijijini kwao.
Mwofuga
alitoa wito kwa serikali kuiangalia eneo hilo la Msamvu Itigi kwa jicho
la pili kwa kufanya operesheni ya nguvu ya kuwaondoa machangudoa hao
eneo hilo lililozungukwa na jamii ili vijana wa kike na wavulana
wasiendelee kuwa na vishawishi vya kuingiza katika vitendo vya kujiuza
na ushoga vingine viwango vya ongezeko la ugonjwa wa ukimwi utaendelea
kuwa juu mwaka hadi mwaka na pengine kushika nafasi ya kwanza kitaifa
kwa maambukizi ya Ukimwi.
Mwofuga
alisema kuwa kakundi hayo sio wote wanaingiliwa kwa kutumia mipira ya
kiume na wanaume bali wapo wanaoingiliwa bila mipira ya kiume kutokana
na sababu moja ama nyingine.
Alitaja
sababu hizo za kuingiliwa machangudoa na wanaume kinatokana na ukweli
kwamba wakati mungine baadhi yao hao machangudoa hukaa muda mrefu bila
kupata mteja na mteja wake wa kwanza kumlazimisha kufanya naye ngono
bila kinga hapo ndipo penye shida na kulazimika kukubali ili kuondoa
mikosi siku husika.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu tangu
kufuatilia mienendo ya machangudoa hao imegundua wanaume wanaofika eneo
hilo la Msamvu Itigi kutozwa fedha kwa viwango tofauti kutokana na aina
ya changudoa waliogawanyika katika makundi mawili.
Makundi
hao ni yale yanayotoa huduma ya ngono ya kuanzia sh2,000 hadi sh 4,000
mteja akilazimika kuingizwa katika kibanda ili akidhi haja zake katika
godoro lililotandikwa chini ya ardhi huku mmiliki wa kipanda hicho
akimtoza changudoa kiasi cha sh1,000 kila mteja atayeingia naye vibanda
vilivyopo nyuma ya vibanda vya biashara wa chakula, vinywaji na n:k.
Kundi
lingine ni lile la machangudoa wa hadhi ya juu ambao wao hutoza dau la
sh5,000 na kuendelea na kumpeleka mteja wao katika vyumba vya kulala
wageni, nyumba ambayo ipo eneo hilo lakini ni hatari endapo watagundua
mteja wao ana pesa na vitu vya thamani kwani wanaweza kumdhuru kwa
kumwekea madawa ya kulevya katika vinywaji ama kumlaghai kwa kumnyonya
matiti yake kabla ya kufanya ngono.
MJUMBE WA BARAZA LA MASHEKHE MKOA WA MOROGORO.
Mjumbe
wa baraza la mashekhe mkoa wa Morogoro, Shekhe Ally Omari Ngarawa
alieleza kuwa yeye kama kiongozi wa dini ya kiislaamu alisikia taarifa
hizo baada ya siku moja kudhuria mchezo wa dhumna uliokuwa ikichezwa
eneo la soko la mkoa wa Morogoro majira ya jioni.
Ngarawa
alisema kuwa ni suala la aibu kwa wao kama viongozi kufumbia macho na
kuwaacha makahama wakiendelea kufanya biashara ya ngono zaidi ya miaka
miwili sasa eneo la Itigi na maeneo mengine.
“Siku
moja nilisikia wanamichezo wa mchezo wa dhumna wakiongea juu ya
biashara ya ngono Itigi lakini nilistuka na kutega sikio kusikia maneno
hayo na sikuweza kuchangia mada hiyo na nilichofanya nilifanya utafiti
wangu kwa wiki mbili ili kubaini ukweli kwa kuchunguza kile nilichosikia
na kweli nilibaini ukweli huo.”alisema Ngarawa.
Ni
kweli ngono inafanyika tena bila kificho, mwanaume akifika hilo eneo la
Itigi huchagua mwanamke anayempendeza naye na kupatana bei kati ya
sh3,000 hadi sh5,000 na wakati mwingine hufikia kiasi cha sh10,000
kutokana na matakwa ya mteja husika.aliema Ngarawa.
Ngarawa
alifafanua kuwa katika utafiti wake huo aligundua kuwa bei hizo hutozwa
kwa huduma mbalimbali kuwa kuanzia sh3,000 hadi sh5,000 mteja hutozwa
kwa kufanya ngono upande wa mbele na kufanya ngono kinyume na maumbile
mteja hutozwa sh10,000 lakini ni lazima mwanaume avae mpira wa kiume.
Alifafanua
kuwa katika biashara hiyo wale wanaotumia kinga kwa maana ya kuvaa
mipira ya kiume hupunguziwa bei na wale wanaume ambao hawataki kuvaa
mipira ya kiume hujikuta wakitozwa fedha nyingine sambamba na wale
wanaowaingilia wanawake hao kinyume na maumbile kujikuta wakitozwa pesa
nono.
Alieleza
kuwa lengo la kufanya utafiti huo alikuwa na maana ya kufikisha ujumbe
kwa waumini wa dini ya kiislamu nyakati za ibada za ijumaa ambako
waumini hufika msikitini kwa uwingi na kutoa mahubiri mara nne ndani ya
mwezi moja.
Kwa
mujibu wa shekhe huyu ambaye ni mwakilishi wa shekhe wa mkoa wa
Morogoro alianza kufanya utafiti februari mwaka huu lengo likiwa kutoa
mafundisho ya namna ya kutojiingiza katika ngono kwani hata kitabu
kitakatifu cha msahafu kinakataza kutokaribia uzinifu kwani inamfanya
binadamu kupata dhambi na kumwingiza katika hukumu ya moto mbele ya
mwenyezi mungu.
Ngarawa
alisema kuwa baada ya utafiti huo amegundua kuwa hali hiyo ya makahaba
inatokana na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wao hasa maisha magumu
hivyo serikali inawajibika kuwaondoa machangudoa sehemu zote za mkoa wa
Morogoro.
Baada
ya kufanya kazi hiyo serikali hiyo inapaswa kuwakusanya katika vikundi
na kuwapatia mitaji ili waweze kufanya biashara na hapo watakuwa
wamerahisisha kupunguza adha ya kupata magonjwa ya maambukizi kama
ukimwi.
Hata
wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika madanguro lazima washirikishe
makundi mbalimbali ya watetezi wa haki za wanawake kama Tamwa, TGNP,
Fame Act, haki za binadamu na haki za watoto na wengine ili kuondoa msuguano ndani ya jamii.
RAIS KIKWETE AELEZA KUPATA UKIMWI NI JAMBO LA KUJITAKIA.
Rais
Jakaya Kikwete akihutubia wananchi wa mkoa wa Morogoro katika uwanja wa
jamhuri alieleza umma wa watanzania kuwa ugonjwa wa ukimwi unatafutwa
na sio ugonjwa wa bahati mbaya.
“Badilisheni
tabia ukimwi ni ugonjwa wa kujitakia kwa baadhi ya watu, sio sifa nzuri
kabisa, unausaka ukimwi kwa kupanga muda, saa, dakika na sehemu ya
kukutana ili kufanya ngono sasa hapo utasema mtu ameupata kwa bahati
mbaya ?.alisema Kikwete.
Kikwete
pia alitumia mwanya huo kuwakalipia viongozi kwa kuwata kuacha woga na
ulegevu katika kusimamia sheria za kulinda zinazoongoza nchi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Morogoro (RPC) Leonard Paulo akizungumza na mwandishi
wa makala hayo ofisini kwake, aliyetaka kupata nini jeshi hilo
linafanya juhudi za kunusuru jamii mzima inayozungukwa na kumbi za
sterehe ambazo zimekithiri kwa vitendo vya kupomoka kwa maadili ya
mtanzania vinavyofanywa na vitendo vya wasichana, wanawake na mashoga
kuuza ngono mjini hapa.
Paulo
alieleza kuwa yeye kwanza ndiyo anapokea taarifa kutoka kwa mwandishi
huyu hivyo kitu cha msingi kwake ni kulifanyia kazi kisha kumpatia
majibu sahihi baada ya yeye kuchunguza na siku ya siku ilete tija kwa
jamii ya Morogoro na taifa kwa ujumla.
"Nimekusikiliza
na nimekuelewa nini unataka kufahamu juhudi za jeshi la polisi katika
kuinusuru jamii na maporoko ya maadili kwa jamii ambazo zinazungukwa na
kumbi za starehe, nalifanyia kazi ili nami nijiridhishe kutokana na
kauli yako ili nikupe taarifa iliyosahihi kwa lengo la kuelemisha
jamii."alisema Kamanda Poulo.
Huu ndiyo mwisho wa makala hayo baada ya kufichua uovu unaofanywa na wanawake na wanaume kufanya biashara ya ngono.
0 comments :
Post a Comment