Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye sifa nyingi nzuri na kuthibitisha hilo haitakushangaza kusikia majina makubwa yanayovuma katika nyanja za medani za siasa, muziki na soka n:k.
Baadhi ya watu maarufu ambao wameiletea sifa nzuri mkoa wa Morogoro ni pamoja na mwanamuziki maarufu Mbaraka Mushekhe, Juma Kilaza huku katika muziki wa kizazi kipya huwezi kukosa kumtaja mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi (Afande Sele) wakati upande wa soka wapo akina Kassim Manga Mlapakolo, Hassan Mlapakolo, Hussein Ngulungu, Gibbson Sembuli, Jella Mtangwa, Zamoyoni Mogella, Malota Soma na Charles Bonoface Mkwasa bila kusahau Mohamed msomali kocha.
Achia mbali wanamuziki na wanasoka kuivumisha Morogoro na kuileta sifa kedekede ndani na nje ya Tanzania wamo wanasiasa walioitangaza vyema wakiwemo Isack Mwesongo,Guntram Itatiro,Alhaji Juma Ngasongwa, na wengine wengi.
Katika makala haya mwandishi wetu anaingalia sifa nyingine zinayoweza kupata mkoa wa Morogoro na kuichafua sambamba na kuitia doa endapo tu viongozi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa hadi Mkoa pengine na Taifa kwa ujumla inaweza kuporoka ghafla kutokana na kuvamiwa na makundi ya machangudoa, mashoga, wasagi na wasenge kukithiri kila penye kumbi za stareha huku kumbi hizo zikiwa zimezungukwa na nyumba zenye watoto wa kike na kiume.
Lakini licha ya sifa hiyo eneo la Msamvu Itigi imekuwa eneo la maficho ya vijana wanaotumia madawa ya kulevya kama kituo kikuu cha kubwia unga mchana na usiku hali ambayo inatishia usalama wa watoto kuwa katika hatari ya kujiingiza katika tabia hiyo.
Halmashauri ya Manispaa kwa sasa imevamiwa na wimbi la makahaba ama maarufu kwa wanawake wanaouza miili yao ama machangudoa wauzaji wa ngono katika kumbi za sterehe zikiwa zimejengwa katika makazi ya watu na endapo hatua za makusudi hazitachukukuliwa kudhibiti makundi hayo basi, hatari itahamia katika kizazi cha watoto wa kike na kiume kujiingiza katika tabia chafu ya kuingia katika kuendesha biashara haramu za ngono.
Kata zilizofamiwa na makundi hayo ni pamoja na Kihonda, Kilakala, Uwanja wa Taifa n:k ambazpo kumbi za sterehe zimezungukwa na makazi ya watu.
Kama viongozi wenye dhamana ndani ya serikali wakishirikiana na viongozi wa dini hawatachukua hatua stahiki basi fedheha na aibu hii hataweza kuikwepa mbele ya viongozi wenzao ndani na nje ya Morogoro kwa kushindwa kudhibiti na kukomesha vitendo vinavyopingana na maadili ya Mtanzania.
Wanawake wakiwa wamegawanyika katika rika la wasichana wenye umri kati ya miaka 18-24, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, wanawake wenye umri kati ya miaka 25-40 kujiingiza katika biashara ya kuuza miili yao katika kona mbalimbali za Manispaa ya Morogoro huku kundi lingine la wavulana nalo likijiingiza katika ushoga na usenge.
Biashara ya ngono imeanza kuota mizizi mkoa wa Morogoro hasa katika miji midogo iliyopo kandokando ya barabara kuu za Mikumi, Dumila na miji mingine kwa makahaba kufanya biashara hiyo.
Tuanze kwa kujiuliza maswali kama kuna kiongozi yeyote kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa hadi mkoa ambaye hajui uchafu huu ?, bila shaka viongozi wa dini ndani ya mkoa wa Morogoro na Taasisi zinazopingana na tabia hiyo nao hawajui kinachoendelea katika maeneo hayo ?, Ni swali linalopaswa kujibiwa kwa viongozi wa serikali, viongozi wa dini, makundi yanayotoa elimu ya kuzuia maambukizi ya ukiwmi na mwananchi mmoja mmoja kiujumla.?
Unaweza kushangaa utaposikia neno Itigi na bila shaka akili itakupeleka Itigi inayoaikia ni Itigi ile inayopatikana katika mji mdogo wa Itigi mkoani Singida tu lakini siyo hivyo kwa Manispaa ya Morogoro neno Itigi inatafsiri nyingine kabisa tena ni aibu kwa vyombo vya dola.
Katika Manispaa ya Morogoro pindi utakaposikia neno Itigi ikivuma eneo la Msamvu Stendi ina maana tofauti tena yakupasa kutega sikio ili kusikiliza hayo maongozi yanagusa Itigi ya Msamvu Morogoro au Itigi ile orojino ya Singida hapo utastaajabu ya Mussa na kuacha ya filauni !.
Itigi ya Msamvu Morogoro ni Itigi wanayopatikana makahama, machangudoa, mashoga, wasenge mahanithi ambapo makundi hayo tayari yameleta athari kwa wanafunzi wa shule za msingi, wanafunzi wa shule za sekondari, wasichana waofanyakazi za ndani, wanawake waliolewa na wavulana kwa pamoja makundi hayo kukaa kando ya magari makubwa eneo la Msamvu Stendi ng’ambo ya maduka ya wafanyabiashara wakiwa wamesimama na nguo za nusu utupu wameegemea malori wakitega mitego ya kuwanasa wanaume ili kuwachagua na kwenda kufanya nao ngono.
Mbaya zaidi katika makundi hayo wapo mabinti wadogo wenye umri wa kwenda shule nao wakigombea wanaume kwa lengo la kufanya nao mapenzi ili wapate fedha jambo ambalo ni aibu kwa viongozi wetu kulifumbia macho sambamba na wazazi wakishuhudia kundi hilo likijiingiza katika biashara hiyo inayotia kinyaa na yenye uvunjifu mkubwa wa matakwa ya dini zetu.
Kundi hilo hujitokeza eneo hilo la Msamvu Itigi mara baada ya kuingia kwa giza kwa lengo la kuwasubiri wateja wao wakiwemo madereva wa malori na makondakta yanaoegesha magari yao eneo hilo kwa ajili ya kupumzika wakitokea Dar es Salaam, ama kuelekea mikoa ya nyanda za juu kusini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Burundi, Congo DRC na wateja wengine wakiwa ni wanaume wenyeji wa mkoa huo na vitongoji vyake.
Moja ya matukio ya kusikitisha yaliyojitokeza katika biashara hiyo ni mwanamke kupoteza maisha baada ya kuharibiwa kizazi chake na mwanaume mwenye maumbile makubwa yaliyosababisha kuvuja damu nyingi baada ya kumlala na kumtelekeza kufuatia ajali hiyo iliyotokea moja ya nyumba ya kulala wageni iliyopo katikati ya Manispaa ya Morogoro.
Tukio hilo lilitokea juni 19 mwaka huu 2014 katika eneo la biashara ya ngono huku tukio lingine likiwa lile la wasichana wawili kufanyishwa biashara ya ngono katika moja za kumbi za starehe wakati wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nao wakijiingiza katika biashara hiyo ya kujiuza katika eneo la Itigi Msamvu.
NAIBU MEYA MSTAAFU.
Naibu Meya Mstaafu katika Manispaa ya Morogoro, Lidya Mbiaji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kuthibiti Ugonjwa wa ukimwi katika Manispaa hiyo anaeleza juhudi walizozuchukua kujaribu kudhibiti hiyo hali lakini juhudi zao hizo ziligonga mwamba tena bila mafanikio.
Mbiaji alianza kwa kusema kuwa katika kizazi kilichopo hakuna kiongozi anayeguswa na jamii moja kwa moja kutokana na baadhi ya viongozi waliopo madaraka kuwa wabinafsi kuliko kutumikia jamii kwa nyasfa za vyeo vyao mbalimbali ngazi ya mtaa hadi mkoa.
“Ni kweli kutokana na uvamizi wa kundi la wauza ngono kuna ongezeko la maambukizi ya ukimwi kutoka asilimia 7.2 kwa mwaka 2013 hadi asilimia 9.2 kwa mwaka 2014 lakini hali hiyo inatokana na ongezeko la takwimu kwa waliopima tu na sasa Manispaa ina asilimia 10.2 kwa maambukizi mapya.”alisema Mbiaji.
Manispaa ya Morogoro kwa sasa imekuwa kitovu cha wauza ngono kutokana na mji huo kuwa njiapanda ya mikoa ya Dodoma, Iringa, Dar es Salaam na nchi jirani za Zambia, Malawi, DRC Congo, Rwanda na Burundi.
Mbiaji alisema kuwa tatizo la kuondoa makundi hayo wakiwemo wanawake, wasichana, mabinti, mashoga na wasenge kunatokana na mkanganyiko wa sheria iliyopo kwani kutokana na sheria hiyo kazi ya kuwaondoa imekuwa ngumu ndiyo maana ongezeko la uchafu ndani ya jamii imeongezeka labda mwenyezi Mungu aingilie kati kuwaondoa jamii hiyo inayoharibu maadili ya mtanzania na Afrika kwa ujumla.
Naibu Meya huyo mstaafu alisema kuwa baadhi ya viongozi wanakerwa na tabia za uchafu ndani ya jamii na kutokana na hali hiyo, aliweza kuunda timu ya kuyabaini makundi ya wafilaji, wasagaji, wasenge, wauza ngono na kubaini kuwa makundi hayo yalivamia Manispaa ya Morogoro na maeneo mengine mwishoni mwa mwaka 2013 wakitokea Dar es Salaam.
“Jiji la Dar es Salaam wamejitahidi kupunguza kwa kuyaondoa baadhi ya makundi lakini yana mtandao mkubwa sana na kutokana na hali hiyo basi sehemu waliyoiona kama inafaa kufanya uchafu wao ni mkoa wa Morogoro na ni kweli makundi hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maambukizi mapya ya ukimya hadi kufikia asilimia 10.2 kutoka asilimia 7.2.”alisema Mbiaji.
Mbiaji alisema kuwa tabia hatarishi zinachangiwa na wamikili wa kumbi za sterehe ambapo machangudoa wamekuwa wakifanya biashara zao za kuuza miili na hali hiyo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nao wamejiingiza huku kundi lingine la wafanyakazi wa ndani na wanawake waliopo ndani ya ndoa wakiwa katika kundi.....
0 comments :
Post a Comment