-->

WAFANYAKAZI 27 WA MUGABE WATIMULIWA KAZI KWA KOSA LA UZEMBE

Rais Robert Mugabe (90) amewatimua kazi wafanyakazi 27 kwenye kikosi cha Usalama kwa kushindwa kuwajibika wakati Rais huyo akianguka.

Uzembe ambao unaonekana kufanywa na jamaa hao ni kitendo cha kushindwa kumdaka kiongozi huyo wakati akianguka, kibaya zaidi ni kwamba alianguka mpaka chini bila msaada wowote kutoka kwao huku wakiwa wamesimama pembeni yake.

Taarifa za kutoka Ikulu ya Rais huyo zinasema huu ni mwanzo tu, uchunguzi unaendelea na wakipatikana wazembe wengine nao watawajibishwa kama walivyofanyiwa hapa.
source:JF
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment