-->

MANJI AONYESHA JEURI YA PESA,AMWAGA MAMILIONI YA PESA

Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji (kulia) amewapa dol 500,000 AU

Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Katibu wa Yanga Dk Jonas Tibohora ambaye naye aliongozana na Manji alisema katika kikao hicho cha 24 cha AU Manji amewasilisha pendekezo hilo akitaka nchi 54 za Afrika kushiriki katika mashindano hayo mafupi kusaka fedha za kupambana na ugonjwa huo hatari unaiosumbua Afrika Magharibi kwa kuchukua washindi wawili wa juu katika kila ligi.
Tibohora alisema katika pendekezo hilo la Manji ambalo nchi zote zililiafiki Manji ametaka mashindano hayo kuchezwa kwa kanda za nchi huzika ambapo mechi hizo zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku kila klabu ikitakiwa kuchangia kiasi cha dola 100000 (shilingi mil 170) kama kiingilio.
Alisema lengo la Manji ni kutaka kuona soka linachangia katika mapambano ya ugonjwa huo ambapo jumla ya kiasi cha dola 10.8 ml zitaweza kupatikana huku mwenyekiti huyo akitangulia kutoa dola 500, 000 kama kianzio. 
"Mwenyekiti amependekeza kwamba kwa kuwa Yanga tunaitwa Young African Football Club jina letu lifanye kitu kuhusu Afrika na kwa kuwa kila kanda za Afrika mfano hii ya kwetu ya Afrika Mashariki tuna utaratibu wetu wa kumaliza msimu, mashindano hayo sasa yafanyike kwa kanda ili kuweza kupatikana muda mzuri wa kuchezeka mechi hizo,"alielezea Tibohora.
"Kwa kuwa mechi hizo zitakuwa zikiendeshwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini Manji ameomba klabu itakayocheza nyumbani itoe nusu ya mapato ya kwenye mechi husika iende katika mapambano hayo hapo pia klabu zitanufaika na nusu ya mapato hayo lakini pia ushindani huo utazinufaisha baadhi ya nchi."
Wakati huo huo, kikosi cha Yanga kimeondoka mchana leo ikiwa na wachezaji wake wote 25 kuelekea Tanga katika mchezo wa Jumatano dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amesema hana majeruhi katika kikosi
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment