KITABU
Ndizi ya Mwisho ( The last Banana ) - Shelby Tucker
RaiaTanzania, Jumatatu 16. 02. 2015
Shelby Tucker ni Mwandishi wa vitabu kadhaa vyahistoria. Kabla ya The Last Banana, ameandika vitabuvingine kama Among Insurgents: Walking through Burma na Burma: The curse of independence. Vitabuhivi vinamfanya awe ni mmoja wa wanazuoniwanaoaminika na kuheshimika. Ni mhitimu wa Chuo Kikuu kikongwe na Oxford. Kitabu hiki kinachohusuAfrika kwa ujumla wake na Tanzania, hususan, kilishawishiwa na urafiki wa mwandishi na mmoja wamwanafunzi wenzake wa Oxford Marios Ghikas. Ghikasni moja ya koo za Kigiriki ambazo ziliishi Tanzania wakati wa ukoloni na kuathiriwa na utekelezaji waAzimio la Arusha. Mwandishi amekuwa akija AfrikaMashariki toka mwaka 1967.
Kitabu hiki kinatoa uhalisia wa utekelezaji wa Siasa yaUjamaa kutoka katika jicho la waathirika. Azimio la Arusha pamoja na mambo mengine liliamua kuwekanguvu zote za uchumi katika mikono ya umma. Hivyomashamba yalitaifishwa, mabenki yalitaifishwa naviwanda na migodi. Familia ya Ghikas ilikuwa inamilikimashamba ya kahawa mkoani Kilimanjaro na pia hoteliya Livingstone ambayo baadaye iliitwa Moshi Hotel. Familia hii ya kigiriki ilinyanganywa mali zote hizikatika utekelezaji wa sias ya Ujamaa. Jina la kitabulinatokana na mwaliko wa Marios Ghikas kwamwandishi, kwamba aje wale ndizi ya mwisho kutokakatika shamba lake kabla ya utaifishwaji kuanza. Ni hadithi nzuri lakini ina kasoro kubwa: imeandikwa kwachuki kubwa dhidi ya Mwalimu Nyerere na sera zake zaUjamaa.
Kwa mfano katika ukurasa wa 235 wa kitabu hiki chenyekurasa 373, mwandishi ametumia maneno makali sanadhidi ya mwalimu kama nukuu ya mtu aliyemhoji. Surayenyewe ya kitabu ameiita Uchawi wa Uhuru naUjamaa. Nukuu hiyo inasema “ Nyerere alisoma kitabukuhusu kujisaidia, akapendezwa. Baada ya hapoakachukua hatua ya kutekeleza sera kuibadili jamiiambayo ilikuwa ni hatari kabisa. Mtu yeyote mwenyemaarifa ya biashara na fedha atashtushwa na matumizi yahovyo, upuuzi na ujinga wa Nyerere” Hakuna linalowezakueleza ukali huu wa maneno dhidi ya Baba wa Taifazaidi ya chuki kubwa iliyotokana na kupoteza mali baadaya utaifishaji.
Kitabu kimesheheni historia kubwa ya utekelezaji waAzimio la Arusha na hasa utaifishaji wa mashamba. Kuna mambo mengi ambayo hatukuyasoma mashulenipia. Mwandishi alifanya utafiti wake wa kutosha nawakosoaji wake ni lazima wajipange kwa kuwa na taarifaza kitafiti. Ndani ya kitabu utawasoma, japo kwa ufupikina Derek Bryceson ambaye alikuwa mmiliki wamashamba (alikuwa na hisa katika shamba la Ol Molog )na baadaye akawa mfuasi mkubwa wa Mwalimu kiasicha kuwa Waziri katika Serikali ya kwanza ya Uhuru. Wazungu wenzake walimwona kama msaliti kwakuchukua upande wa haki “Breyceson alichukua uraiawa Tanzania na akajiunga na Nyerere jambo lilileta chukikubwa kutoka kwa wazungu wa Tanganyika”.
Ndani ya kitabu pia utasoma kuhusu Elias Mshiu ambayealikuwa Mtendaji Mkuu wa Chama cha WakulimaTanzania na ambaye alikuwa mpingaji wa sera yaUtaifishaji kiwango cha kuonekana ni mtetezi wawazungu. Vile vile Edwin Mtei. Kuna simulizi yaugomvi kati ya Mtei na John Malecela. “ Edwin Mteimwafrika mwingine aliyepinga utaifishaji alizuiautaifishaji katika mkoa wa Arusha. John Malecela Alikuwa akiunga mkono kwa nguvu utaifishaji huo akiwa waziri wa kilimo. Mwaka 1978 Serikali ya Uingerezailitoa msaada kwa Tanzania ili kulipa fidia wakulima waKiingereza watakaoathirika na utaifishaji. Mteialishawishi waingereza kutumia msaada huo kujengahostpitali Mbeya na barabara ya Makambako – Songea. Malecela alikasirika sana na Nyerere alishangazwakwanini hakushirikishwa. Mtei aliwajibu kuwa mpangowa maendeleo uliokuwa ukitekelezwa ulikuwa unatakakupanua huduma za afya na mtandao wa barabara na nikazi yake yeye Waziri wa Fedha kutafuta fedha zakutekeleza Mpango wa Maendeleo.”
Kuna simulizi pia la Peter Kisumo alivyochukua hoteliya The Livingstone iliyokuwa inamilikiwa na Ghikas nakuifanya kuwa chini ya Shirika la Utalii Tanzania. “ ….Peter Kisumo akiwa na watu wengine kama 12 hiviwalikuja Hotelini na kumwambia Marios kwamba Hoteliile inachukuliwa na Shirika la Utalii Tanzania nakwamba awalipe wafanyakazi mishahara yao yote namalipo mengine ya kuachisha watu kazi. Mariosakawaambia kuwa hawana mamlaka ya kumlazimishayeye kulipa wafanyakazi wake. Kisumo alibadili Jina la Hotel na kuita Moshi Hotel. Mwandishi alipokutana naKisumo mwaka 1998, Kisumo alimweleza kuwa WaziriMkuu wa Uingereza Harold Wilson ndiye aliyemshauriMwalimu Nyerere kutaifisha mali za walowezi wakizungu waliokuwepo Tanzania. Kuna simulizi nyingisana katika kitabu hiki. Utawakuta kina Arnold Kilewoalipokuwa meneja wa Shamba la Kahawa huko Narumuna wengine wengi ambao walinyanganywa pasi zao zakusafiria na kufukuzwa nchini. Historia nzuri kwa vijanawa sasa ambao hawakuona utekekelezaji wa siasa yaUjamaa.
Kitabu hiki pia kina simulizi za Zimbabwe, Sudan yaKusini, Ethiopia na Zambia. Vile vile ni kama hadithi yamaisha ya Mwandishi katika Afrika Mashariki. Mwandishi alifunga ndoa huko Zanzibar wakati wautawala wa Aboud Jumbe. Kuna hadithi ya kuchekeshaya namna mchungaji wa kanisa la Anglikana alipotakakibali kutoka Ikulu kwa ajili ya ndoa ya mwandishi. Mwanasheria Mkuu wakati huo Bwana Dourado ndiyealimsaidia kwa cheti kusainiwa na Hassan Nassor Moyoaliyekuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais. Sikuelewa nikwanini ndoa ilihitaji kibali cha Ikulu ya Zanzibar.
Mwandishi, ambaye familia yake iliwahi kumilikiwatumwa (descendet of slave owners), ana mashakamakubwa sana na uongozi wa Mwalimu Nyerere. Anaonyesha namna Ujamaa ulivyoleta umasikini, Nyerere alivyoweka ndani watu kwa sheria ya preventive detention na Nyerere alivyosaidia mapinduzi ya kijeshihuko Seychelles, Zanzibar na Comoros. “ Hata hivyomamilioni ya Watanzania wanamwabudu Nyerere kamaMusa aliyewatoa kwenye utumwa, kama mwalimu waona Baba wa Taifa. Kizazi kijacho cha Watanzaniawataendelea kumwona hivyo?” anamalizia Mwandishi.
Mfuasi wa Mwalimu Nyerere kama mimi atachukizwana baadhi ya sentensi na hukumu dhidi ya Mwalimukatika kitabu hiki. Hata hivyo ni kitabu muhimu kusomaili kuona namna waathirika wa utaifishaji walivyoonasiasa ya Ujamaa. Swali la msingi ni, kwanini tulipoamuakubinafisha kila kitu tulichotaifisha na tulichojengawenyewe bado tulirejea kufaya makosa yale yale? Wakati utaifishaji uliumiza wachache na ‘kutajirisha’ wengi. Ubinafsishaji ulitajarisha wachache kwa maliiliyochumwa na wengi. Nini kinafuata?
0 comments :
Post a Comment