Jioni hii kwenye mgahawa niupendao Dar
walitinga washabiki wa Al Ahly waliosafiri toka Cairo kuja kuishangilia
timu yao. Wananiambia wamekuja Dar kuishangilia timu yao itoke sare au
ifungwe moja tu! Wanasema wana uhakika wa kuifunga Yanga Cairo,
wasichokijua ni idadi ya magoli...! Mtazamo
wangu; Yanga wamecheza vizuri. Wamewalazimisha Al Ahly kwao kufanya
mawili magumu; kuzuia wasifungwe na lazima wafunge. Yanga hawatakiwi
kabisa kujihami. Wacheze kama vile wao ndio wenye kuhitaji goli moja. Ni
ushauri tu bila kujali kuwa anayeutoa ni Simba damu... CHANZO:Maggid MJENGWA, Dar.(P.T)
0 comments :
Post a Comment