-->

MAREKANI YATANGAZA KUPEPERUSHA BENDERA YA NCHI YAO NUSU MLINGOTI KUMUENZI NELSON MANDELA


MZEE NELSON MADIBA MANDELA. 

MARAa tu baada ya kupokea habari juu ya kifo cha Madiba Alhamis jioni, rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba na rambi rambi zake  akisema Mandela aliishi na kuifanya ndoto yake kutimia ya kuwa na Afrika Kusini huru na yenye demokrasia.
Rais Obama alikwenda kwenye  chumba cha White House anakozungumza na waandishi habari wa Ikulu mara tu baada ya kupokea taarifa  za kifo cha  Mandela zilizotangazwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Barack Obama
Obama alisema  marehemu Mandela katika uhai wake aliishi kwa kupigania  ndoto yake na akaitimiza. Alifanikiwa katika mambo mengi kuliko inavyotegemewa kwa mtu yeyote. Leo hii amekwenda nyumbani. umempoteza mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa, mtu  jasiri, binadamu mzuri ambaye tumeishi naye dunia hii. Wasifu wake utadumu milele.”

Rais Obama  pia aliamrisha bendera zote za Marekani zipepee nusu mlingoti hadi  Jumatatu jioni.

Viongozi wengine wa dunia wanamkumbuka mpiganaji dhidi ya ubaguzi wa rangi na rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela. Marais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, Bill Clinton, George W. Bush na George H.W. Bush pia walimsifia bwana Mandela kama kinara wa uhuru, utu na mwanaharakati wa kutetea usawa.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -Moon amesema amesikitishwa sana na kifo chake na ametoa mwito kwa watu kufuata nyayo za mzee Mandela. Mkuu wa tume ya Jumuiya ya Ulaya Jose Manuel Barosso alisema Bw Mandela alibadilisha historia ya dunia wakati waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema  marehemu Mandela  alikuwa mtu mwenye  maono aliyepinga ghasia.

Na huko Afrika Kusini umati mkubwa wa watu umekusanyika nje ya nyumba ya Bw. Mandela mjini Johanesburg kuimba na kucheza, kutoa heshima zao za mwisho wakifuata utamaduni wa Afrika Kusini baada ya kifo chake.

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment