Mwili wa jambazi hilo |
Kijana
mmoja ambaye hajatambulika jina lake mwenye umri kati ya miaka 26 hadi
30 ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa na wenzake wakijaribu kuvunja
duka maeneo ya Shunu, kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.Tukio
hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo ambapo jambazi
hilo likiwa na wenzake watatu liliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na
Wilson Masolwa (63) mkazi wa mtaa huo ambaye alijeruhiwa kwa mapanga.
Mtu
huyo ameuawa kwa Bunduki aina ya Shortgun ambayo hata hivyo wenzake
waliipora baada ya kumkata mapanga Masolwa na kupoteza fahamu.
Akizungumzia
tukio hilo mmiliki wa nyumba hiyo Yasinta Patrick (32) amesema mtu huyo
na wenzake walivamia katika nyumba yake, ambayo ameipangisha kwa
wafanyabiashara wawili wa kutoa na kutuma fedha kwa njia ya mtandao.
Mmiliki wa nyumba iliyovamiwa Bi Yasinya Patrick |
Kwa
upande wake Masolwa amesema baada kusikia kelele alifika katika eneo
la tukio na ndipo majambazi hao walianza kumkata mapanga kabla ya yeye
kumpiga risasi ya kichwa mmoja wao na kufariki dunia papo hapo.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba Masolwa amefikishwa katika Hospitali
ya wilaya ya Kahama kupatiwa matibabu na kuruhusiwa na kwamba hali yake
inaendelea vizuri.
Kamanda
Kihenya mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya
ya Kahamaa na kwamba jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwabaini
na kuwakamata wahusika watatu waliotoroka ikiwa ni pamoja na bunduki
waliyoipora.
Maduka yaliyokuwa yakifanyiwa uhalifu na majambazi hayo |
Mmiliki wa Blog hii na Mtangazaji wa Redio Kahama FM Faraji Mfinanga akimuhoji Mzee Masolwa |
CHANZO DUNIA KIGANJANI BLOG
Blogger Comment
Facebook Comment