DALILI ZA MTU MWENYE MIMBA
Dalili ya wazi kuwa mimba imetungwa ni kukosa kupata hedhi. Hii ni kwa sababu ukuta wa mfuko
wa kizazi hautoi damu mwanamke akiwa na mimba. Utando laini unabaki ndani ya mfuko wa
kizazi na unatengeneza kiota laini kwa ajili ya mtoto kukua. Kukosekana kwa hedhi haina maana
kuwa umepata mimba. Wasichana waliobalehe wanaweza kuwa na hedhi isiyo ya kawaida. Kwa
miaka mingi siku za hedhi kwa baadhi ya wasichana balehe, zinaweza kuchelewa au zikakosekana
mwezi mzima bila sababu yoyote.
Dalili nyingine za mimba:
• Matiti kuwa laini
• Kichefuchefu (hali ya kutaka kutapika) na kuwa na mate mdomoni.
• Uchovu (kujisikia umechoka sana)
• Kutaka kukojoa mara kwa mara
• Kupendelea kula vitu fulani,wakati mwingine visivyo vya kawaida.
Wanawake wachache huwa hawaoni dalili zozote kati ya hizo hapo juu. Kwa mfano, wanawake
wengine hutoa damu kidogo sana wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya mimba zao na hivyo
wanaweza kufikiri hedhi imekuwa na damu kidogo kuliko kawaida.
Kama huna uhakika kuwa umepata au hujapata mimba, unaweza kufanya kipimo cha mimba.
Katika sehemu nyingine, unaweza kununua kipimo cha mimba kwenye maduka ya dawa. Vilevile,
unaweza kufanyiwa kipimo cha mimba kwenye kliniki. Mara nyingine kipimo kinafanywa kwa
kupima mkojo na unaweza kugundua viini fulani ambavyo vinatengenezwa na mwili wakati wa
mimba. Dakitari au nesi wa kituo cha afya anaweza vilevile akakufanyia uchunguzi wa mwili ili
kuona kama una mimba au la.
Mimba inachukuwa wiki 40 kabla ya mtoto kuzaliwa(toka mwanzo wa hedhi yako ya mwisho).
Hadi utakapokosa hedhi yako – kama siku 28 baada ya siku ya mwisho ya siku zako za hedhi
iliyopita – kibonge cha seli nyingi, yaani kiinitete kitakuwa kinakua katika mfuko wa kizazi kwa
karibu wiki nzima.
Kiinitete kinakua haraka sana. Wiki sita baada ya hedhi yako ya mwisho, ubongo na uti wamgongo vinakuwa vimeanza kutengenezwa na moyo unaanza kupiga. Katika wiki 9 kiinitete kinaitwa fitasi. Katika wiki ya 12 fitasi inatambulika kama binadamu ila inakuwa na kichwa kikubwa. Katika wiki 20 (miezi 5) mwanamke anaweza akajisikia fitasi inachezacheza au kuzunguka ndani ya tumbo lake. Fitasi inaweza kugeuka au kusogea na inaweza pia ikashituka kukiwa na kelele zenye sauti ya juu.
0 comments :
Post a Comment