Na Ramadhani Bendera
.Kwa tathmini ndogo niliyoifanya kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watangaza nia nimebaini yafuatayo; (1)CCM ndicho chama pekee cha siasa nchini chenye idadi kubwa ya makada wenye ushawishi mkubwa jambo linalopelekea kufikiriwa kuendelea kutawala kwa miongo mingi ijayo hvyo wapinzan wajipange.(2)Kwa idadi hii ya watangaza nia yaonesha wazi kuwa hakuna mwenye uhakika na kiti cha uraisi.(3)Kutangaza nia kumetumiwa kama njia ya kukwepa fedheha kubwa kwa gharama ndogo na baadhi ya wagombea waliofanya vibaya katika majimbo yao.(4) Idadi kubwa ya wagombea walikuwa watumishi katika serikali inayoondoka madarakani na wanadai wanao muarobain wa matatizo ya watanzania,so napata shida juu ya uwezo wao wa kuishawishi serikali kuchukua maoni yao.(5) Masharti mepesi katika katiba za vyama na ile ya nchi zimeongeza utitili wa wagombea.
0 comments :
Post a Comment