Mfano wa banda la ghorofa lenye nafasi ya kuku 100 (Picha na Mamachi Agribusiness) |
Huu ni ufugaji wenye tija na katika eneo dogo.
*Eneo linalohitajika ni mita mbili (2), Kwa maana ya Urefu wa mita mbili(2) na Upana wa mita moja(1).
*Kinakachofanyika katika hilo eneo ni ujenzi wa ghorofa/shelves tano(5) kwenda juu kwa ajili ya kufugia kuku.
*Urefu unaoshauriwa wa kila shelf/chumba kimoja ni futi moja na nusu hadi mbili.
*Katika kilachumba/shelf unashauriwa kuweka kuku ishirini, kwa maana ya kuku 10 katika eneo la mita 1.
*Ukichukua idadi ya kuku katika kila chumba (20) mara idadi ya vyumba 5, watapatikana kuku mia(100) katika eneo la mita 2.
*Kumbuka kuwa unaweza kufanya mabadiliko mengine kulingana na eneo utakaloweka ghorofa la kuku.
Vifaranga vya kuku huwekewa chakula katika vyombo vidogo |
Usiogope, kuna nafasi ya kutosha kuruhusu ukuaji wa kuku |
0 comments :
Post a Comment