-->

BARACK OBAMA ARUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA KATIKA MAJIMBO YOTE YA MAREKANI





Headlines kubwa za leo zinatoka nchini Marekani ambako dakika chache zilizopita Rais Barack Obama ametangaza kuhalalishwa kwa ndoa za jinsia moja katika majimbo yote 50 ya Marekani.

Kuanzia leo mtu yoyote anaeishi Marekani na aliyee kwenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ana haki zote za kisheria kuingia katika ndoa na mpenzi wake, na haki hii itakua sawa kama vile ilivyo kwa watu wenye mahusiano ya kawaida ya kimapenzi.

Maamuzi haya yametokana na raia wengi wa Marekani kupiga kura kuipinga sheria ya awali ambayo ilikua imehalalisha ndoa hizi kwa majimbo machache kwa kudai kuwa kitendo hiki ni ubaguzi wa haki na kinaenda kinyume na katiba ya nchi inayosema kila Mmarekani ana haki sawa.

Awali, majibo 36 kati ya majimbo 50 yalikua yamehalalisha ndoa hizi huku wapenzi wanaume wa jinsia moja wengi walikua wakionekana kupendelewa kuliko wapenzi wanawake wa jinsia moja .
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment