-->

TETESI ZA USAJILI KATIKA SOKA BARANI ULAYA LEO HII

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 02.06.2015
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 26 amewaambia marafiki wake kuwa anataka kuondoka Chelsea na kurejea Spain (Sun), Patrick Vieira hajaambiwa lini atapata fursa ya kujadili nafasi ya ukocha wa Newcastle. Vieira, 38 ambaye kwa sasa ni mkuu wa kikosi cha vijana chipukizi wa Manchester City, ni miongoni mwa wanaotajwa kuwania nafasi hiyo pamoja na Steve McClaren (Daily Telegraph), Brendan Rodgers ataendeela kuwa meneja wa Liverpool, lakini ikiwa tu atakubali sera ya usajili isimamiwe na wamiliki wa timu (Daily Mirror), mshambuliaji wa Dynamo Kiev Andriy Yarmolenko amesema yuko tayari kuhamia katika Ligi kuu ya England, huku Liverpool na Tottenham wakionesha kumtaka (Daily Mail), Manchester United wanaamini kuwa wapo katika nafasi ya mbele kumsajili Dani Alves, 32, kutoka Barcelona, iwapo Louis Van Gaal atamtaka beki huyo wa kulia kutoka Brazil (Guardian), Manchester United wamethibitisha nia yao ya kumtaka Bastian Schweinshteiger, lakini wataamua kumfuatilia Morgan Schneiderlin wa Southampton iwapo mpango wao huo haiutakamilika (Daily Star), Real Madrid wanataka kuanza mazungumzo ya zaidi ya pauni milioni 45 na Liverpoool ya kumsajili Raheem Sterling, 20 (Sun), mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 26, atajadili ni nafasi gani atacheza, na atacheza mara ngapi, kama sehemu ya mkataba wake na Arsenal (Daily Mirror), Liverpool huenda wapo karibu kumsajili James Milner kutoka Manchester City, lakini hawapo tayari kufikia madai ya Aston Villa ya kumsajili Christian Benteke. Benteke, 24, ana kipengele cha ununuzi cha pauni milioni 32.5 (Independent), Benteke atawaambia Aston Villa kuwa anataka kuondoka ili aende timu inayocheza UEFA, licha ya Villa kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo (Times), beki wa Juventus Giorgio Chiellini, 30, amesema hana tatizo na kupeana mikono na mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 28, katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya siku ya Jumamosi. Wawili hao watakutana kwa mara ya kwanza tangu Suarez alipomng'ata Chiellini katika Kombe la Dunia (Independent), mabeki Aly Cissokho, 27, Phillipe Senderos, 30 na Matt Lowton, 25 ni miongoni mwa wachezaji watakaouzwa na Aston Villa katika kipindi cha uhamisho (Birmingham Mail), Everton wameanza mazungumzo na kiungo Tom Cleverly, 25 ambaye mkataba wake na Manchester United unaisha msimu huu (Liverpool Echo), beki wa Saint Etienne Franck Tabanou anataka tu kuhamia Swansea msimu ujao, kwa mujibu wa wakala wake (Wales Online), kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko, 25, anataka kuhamia Chelsea msimu ujao na anadhani Jose Mourinho anamfuatilia (Daily Express), kiungo wa Paris Saint-Germain, Thiago Silva, 30, anaamini kuna uwezekano mkubwa wa Carlo Ancelotti kurejea AC Milan (Goal.com), na kiungo Yaya Toure, 32, ameamua kubakia Manchester City baada ya kuwa na mazungumzo na mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak (Daily Star). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Cheers!!
 KWA MAHITAJI YA BLOG PIGA 0714557223 SASA HIVI ILI UJIPATIE BLOG YAKO KALI NA YENYE MVUTO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment