-->

JACOB MALIHOJA:UKWELI UMESHAUSHINDA UONGO! – SEHEMU YA TATU UONGO WA NYERERE KUMKATAA LOWASSA NAO UMEKUFA NI MJINGA TU ANAWEZA KUENDELEA NA UONGO HUO

(Pichani Mhe. Lowassa akiwasilisha tuzo kwa Mwalimu aliyokwenda kuipokea kwa niaba yake nchini Ugiriki)
Na Jacob Malihoja
Kuna wajinga fulani walijaribu kutunga hii na kuisambaza, kwa bahati mbaya sana hata historia hawaijuia. Wamejaribu kumhusisha Mzee Yusuf Makamba na Samueli Sitta kwenye kikao cha NEC cha mwaka 1995 ili kuhalalisha uongo wao uonekane ni kweli wakati Yusuf Makamba na Samuel Sitta hawakuwa wajumbe NEC mwaka huo na hawakuwepo kwenye kikao hicho. Hebu soma uzushi huu halafu endelea na Mada;
==========================
“Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu.” – Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere,
=============================
Hivi Ilikuwaje baba wa taifa awanukuu watu ambao sio viongozi wa juu wa Chama, wala hata kwenye kikao hawapo na awaache vigogo waliokaa jirani yake ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Mzee Alli Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu wa CCM Dr. Laurence Gama na wengine waliokuwepo? ..
=============================
Ukweli ni kwamba baba wa taifa hajawahi kumkataa Lowassa, ni uzushi tu wa watu, lakini jambo la kushukuru watazania wameshafunguka, hawataki tena kusikiliza uongo, majungu na fitina. Hoja hii ya Mwalimu Kumktaa Lowassa imeshakufa, Ukweli umeushinda uongo.
Lowassa ni mmoja wa watu walioaminiwa sana na mwalimu na ndio maana katika nyakati tofauti chini ya uenyekiti wa baba wa taifa Chama cha mapinduzi kilimpa majukumu Mbali Mbali mazito katika chama. Lowassa aliteuliwa kuwa katibu Msaidizi wa Wilaya, Katibu wa wilaya, katibu wa mkoa, msaidizi wa Mzee Daudi Mwakawago, msaidi wa Mzee wa Horace Kolimba na msaidizi wa Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Kwa namna Nyingine ndio alikuwa mtendaji wa majukumu wa viongozi hawa wa kitaifa. Katika uhai Wake baba wa taifa alishuhudia Mzee ali hassan mwinyi akimteua lowassa kuwa Mkurugenzi wa AICC, kwa utendaji mzuri mwaka mmoja tu baadae alimteua kuwa waziri na kumpa wizara mbali mbali, hadi alipoingia mzee mkapa Madarakani, ambapo nae alimteua Wizara Mbali Mbali kipindi chote hicho baba wa taifa alikuwa hai, kaama angekuwa hampendi Lowasa na kumuagalia kwa sura ambayo wapuuzi wachache wanamuangalia Lowassa asingekubali apewe nafasi nzito zito mbali mbali alizopewa. Kana kwamba haitoshi Mzee Mkapa akiwa rais alipokuwa akizindua mradi Mkubwa wa maji wa chalinze aliemsifia Lowassa waziri wa maji na mbunge wa jimbo hilo jakaya Mrisho kikwete kuwa wamelelewa na kukulia ndani ya Chama Cha Mapinduzi;
“Hawa (LOWASSA NA KIKWETE) ni viongozi ambao wamelelewa na kukulia ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Hawa wawili ..lakini nasema kwa uaminifu wao huo na utendaji bora kutokana na malezi ndani ya Chama Cha Mapinduzi .. hawa wanastahili sio tu sifa lakini shukrani zetu, nyinyi .. wananchi wa Chalinze lakini wananchi wa taifa hili ..na mimi kwa niaba yenu nawaambia wazi wazi asanteni sana wembe ni ule ule, endeleeni” alisema Mkapa.
NI MJINGA TU ANAWEZA KUENDELEA NA UONGO HUO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment