Na Jacob Malihoja
Baada ya kuona Uongo, Uzushi, Fitina na majungu yao ya siku zote yamedunda, sasa wanajaribu kusambaza habari za mkutano wa NEC wa mwaka 2011 wakiwa wamebadili dhana ya Mkutano huo na kuijengea nyama za uongo, majungu na fitina kama walivyozoea wakiwa na lengo la kuchoganisha na kupotosha. Jamaa hawa wanashindwa kuelewa kuwa Watanzania wameshawashitukia, hawawasikilizi tena, sana sana wanawaona ni wajinga tu. Hawatambui kuwa hali ilivyo, na watanzania wanavyowachukulia, hata uzushi huo pia ulishakufa hata kabla hawajauleta mitandaoni.
Kuna wale waliosimama muda mrefu na Suala la Richmond wakidai ni ufisadi wa Lowassa .. hoja hiyo nayo imekufa, watu hata muda wa kuwasikiliza kwa sasa hawana .. na imefika mahali wanaoendelea kukazana na hoja hizo ambazo wameshindwa kuwapatia watanzania ushahidi wake, wanaonekana ni wajinga mbele ya macho ya watanzania.. kwasababu huwezi kumtuhumu mtu miaka kadhaa kwa tuhuma ambazo ushahidi huleti. Watanzania wanampenda zaidi Lowassa sasa hivi kwasababu wameona anaonewa kwa kuzushiwa uongo wa kila aina, na ni hulka ya wanadamu kuwa upande wa mtu anayeonewa.
Kuna wale ambao wamekuwa wakitegemea ripoti ya Mwakyembe itetee tuhuma zao dhidi ya Lowassa.. yani hadi huwa nawaonea huruma .. ukiacha shaka ya kwanza ambayo ni kitendo cha kamati hiyo kuacha kumhoji Mhe. Lowassa ambaye ndiye mtuhumiwa wao mkuu, Shaka ya pili ya kutotumia maelezo ya Lowassa aliyoyawasilisha kwa Spika wa bunge .. Ripoti ya Mwakyembe haijasema wala haijathibitisha katika kipengele chochote kuwa Lowassa ni fisadi, au Kuwa Lowassa alikula hela ya Richmond au kuwa Lowassa ndio mwenye Richmond .. hakuna kipengele kama hicho .. mwenye nacho akilete kujibu hoja hii.. Kipengele ambacho kutokana na uelewa mdogo kinawachanganya watu, kipengele ambacho hakina weledi wa Kisheria ingawa ripoti ilisimamiwa na kuandaliwa na Mwanasheria aliyebobea .. ni hiki;
================================
“Lakini Mhe. Dk. Msabaha (Mb), baada ya mahojiano chini ya kiapo, akaiuma sikio Kamati Teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe, “Bangusilo” kwa lugha ya Kizaramo.
Maelezo hayo ya ziada nje ya kiapo ya Mheshimiwa Waziri yaliyotoa ujumbe kuwa “si yeye ila mkuu wake wa kazi”, yalioana na maelezo aliyoyatoa Balozi Kazaura nje ya kiapo tarehe 30 Novemba, 2007. Mara baada ya kumaliza mahojiano kwa kiapo na Kamati Teule, Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa “Bwana Mkubwa” na “mshiriki wake mkubwa kibiashara”, akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb).
==================================
Hapa wanasheria wanaacha kuamini maelezo yaliyotolewa chini ya kiapo na kuamini “Kuumwa sikio” nje ya kiapo, baada ya kikao.. Kulikoni? .. lakini Mbaya zaidi Ni Pale ambapo wanasheria wanaongeza maneno yao wenyewe “akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb).” Nani aliwaambia wanamaanisha hivyo? Wanasheria hawa hawakujiuliza Kuna “Wakuu wangapi wa kazi” au kuna “Mabwana wakubwa wangapi” juu waziri au balozi Kazaura . .Mpaka wakakimbilia wao kusema “Waziri mkuu na Mhe. Rostam Aziz” .. Kulikoni Hapo? Nani aliwaambia kuwa bwana mkubwa au Mkuu wa kazi anayekusudiwa hapo ni Waziri Mkuu?
Hii bado haiwezi Kuwa Ushahidi, kwanza ni Maneno Yaliyotolewa nje ya kiapo .. pili ni maneno tu ambayo hayakuwa na kielelezo chochote kuthibitisha huko kung’atwa sikio kama ni kweli.
Hoja ya ufisadi wa Lowassa kwasababu ya Richmond ilishakufa mana hata ripoti yenyewe yenyewe imeshindwa kuthibitisha. Na Watanzania kwa sasa wanapomuona mtu anasimama na hoja hiyo wanamuona ni mjnga tu.
Tena hasa watanzania wanapoona Rais wa Marekani Barack Obama kaja mzima Mzima kuja kuzidua na kusifia mitambo kuwa ni ya Kisasa, mitambo ambao wazushi walieneza habari kuwa ni mibovu na imeingia nchini kwa kashfa, Rais Huyo Akiongozana na Waziri wa mambo ya nchi za nje. Jambo ambalo kwa Marekani kiongozi kujiusisha na kashfa nzito ya ufisadi Rais Lazima uondoke.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Edward Ngoyai Lowassa
Uchambuzi Umeandaliwa na Jacob Malihoja
Mwanaharakati
0 comments :
Post a Comment