Hilii
ni funzo kwa shirikisho letu la soka la Burundi Mze Reveriano na crew
yake watazame vile wanaweza kujifunza kitu kutokana na haya...kwa mtu wa
akili amesha elewa nini hapa Watanzania wanalenga...isome hii
**********************************
Shirikisho la soka nchini jirani ya Tanzania (TFF) limepitisha azimio la kila mchezaji wa kigeni kulipa dola 2,000 ( wastani wa milioni 5) kwa kila msimu atakaocheza ligi kuu ya Tanzania.
Kiasi hicho cha pesa kitaanza kulipwa katika msimu ujao wa ligi kuu ya nchini humo wa 2015/2016 .
Wachezaji wa kigeni waliosalia kuendelea kuchezea timu zao na wale wanaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao watalazimika kulipa kiasi hicho cha pesa.
Msemaji na afisa habari wa shirikisho hilo la soka (TFF), Bw Baraka Kizuguto amesema maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilichoketi Jumamosi huko visiwani Zanzibar ni kuwa kiasi hicho cha pesa kitakuwa ni kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini mwao Tanzania.
Katika miaka ya nyuma, wachezaji wa kigeni kutoka nchi mbalimbali, hasa za Afrika ya Mashariki kama Kenya, Uganda, Rwanda pamoja na Burundi walikuwa hawatozwi kiasi chochote cha pesa licha ya kulipwa mamilioni.
Bw Kizuguto amesema fedha hizo zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu ujulikanao kama (Football Development Fund).
Source : BBC Swahili

0 comments :
Post a Comment