TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 16.06.2015
Chelsea huenda wakacheza mechi zao za nyumbani ugenini kwa angalau misimu miwili kama sehemu ya kuongeza idadi ya watazamaji kufikia 60,000 Stamford Bridge (Guardian), maneja wa Juventus Massimiliano Allegri amesema itakuwa vigumu kukataa kama dau la maana litatolewa kwa kiungo Paul Pogba. Pogba, 22, amehusishwa na Chelsea, Manchester United na Manchester City (Gazzetta dello Sport) Manchester United wamewaambia Real Madrid kuwa hawatafikiria dau lolote chini ya pauni milioni 25 kumnunua kipa David De Gea (Sun) mshambuliaji Harry Kane, 21, ameshauriwa na Fabrice Muamba kuwapuuza Man Utd na kubakia Tottenham (Express), Monaco wanawataka kwa mkopo kungo wa Chelsea Mario Pasalic, 20 na Charly Musonda, 18, kama sehemu ya mkataba wa Chelsea kumchukua Radamel Falcao kwa mkopo (Telegraph), kocha wa makipa wa Chelsea anaamini kuwa Petr Cech, 33, anataka kwenda Arsenal (Mirror), Liverpool wataongeza dau lao kutaka kumsajili beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne baada ya pauni milioni 10 kukataliwa (Liverpool Echo), wakala wa Roberto Firmino amesema mchezaji huyo wa Hoffenheim ambaye amehusishwa na kuhamia Manchester United, amethibitisha kuwa mchezaji huyo anataka kuhamia Uingereza lakini mkataba wowote utafikiwa baada ya michuano ya Copa America (Bild), Man Utd lazima walipe pauni milioni 35 kama wanataka kumsajili beki wa Valencia Nicolas Otamendi, 27 (Mirror), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa Barcelona Gerrard Deulofeu (Star), Liverpool huenda wakamsajili beki wa Charlton Joe Gomez, 18 kuziba nafasi ya Sebastian Coates ambaye anatarajiwa kwenda Sunderland (Guardian), Tottenham wanakaribia kumsajili beki Kieran Trippier, 21, kutoka Burnley. Liverpool, Newcastle, West Ham, Bournemouth na Southampton pia wanamtaka (Mail), Spurs pia wanataka kumsajili Mohamed Salah, 23, kutoka Chelsea (Evening Standard), Inter Milan wameanza tena mazungumzo na wawakilishi wa Stevan Jovetic na wana uhakika wa kukamilisha mkataba huo kutoka Manchester City (GIanluca di Marzio). Tetesi nyingie kesho tukijaaliwa. Cheers!!
0 comments :
Post a Comment