Na Jacob Malihoja
Kitendo cha maelfu ya watu kumiminika kumdhamini Mhe. Edward Lowassa kila aendako na ushauri wa baraza la wazee wa chama la Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Msekwa kama ilivyoripotiwa na vyomba vya habari, ni uthibitisho tosha kuwa ukweli umeushinda uongo.
Nimewahi kuandika na kusisitiza mara kadhaa kuwa Ukweli Utaushinda Uongo, Nimewahi kueleza na kusisitiza mara kadhaa kuwa mihimili mikuu ya mahasimu wa lowassa ni Uongo, Uzushi, Majungu na fitina. Jamani Ukweli ni RUNGU zito sana limepondaponda uongo na uzushi wote anaozushiwa Lowassa na sasa wazushi wanapata aibu, wanatapatapa labda tujaribu kutunga hili, labda tujaribu kuzusha lile. Kwa wale waliokuwa wakifuata uongo huu na kushiriki kuusambaza bila kujua lakini wana hekima baada ya kugundua Lowassa anazushiwa tu wameachana na uongo na kuhamia kwenye kweli, tupo pamoja sasa. Hawa Nawapongeza sana na Mungu awabariki kwa hekima na ujasiri walionao. Si jambo la aibu, bali ni la kishujaa na hekima kurudi kwenye kweli hata kama uliponda sana, lakini ni ujinga kuendelea kusambaza uongo hali umeshajua kweli.
Walikuja na hoja Lowassa mgonjwa, wakazusha mengiii..wenginekwa ujinga tu wamejaribu kutumia vipande vya magazeti ya udaku, wengine wamejaribu kufanya video slow motion, wengine wamejaribu kutafuta hata vipande vya video Lowassa akisita kidogo kutembea au akiyumba kidogo .. basi wanajengea hoja.. lakini ukweli huwa unashinda wakati wote, wamemuona Lowassa anakimbia Kilometa Tano, Wengine wamemuona anashika chepe Kumzika Mufti Simba .. pia wanamuona Lowassa katika ratiba ngumu ya kuzunguka nchi nzima bila kumpumziak hata siku moja kutafuta wadhamini na kufanya mikutano ya kuwashukuru....wanamuona anachapa mwendo tu ..hoja hiyo ya ugonjwa imekufa, Walikuja na hoja Lowassa anabebelea watu kujaa kwenye mikutano yake, wameshindwa kuthibitisha, hoja imekufa, Walikuwa na hoja Lowassa analipa watu wajae kwenye mikutano yake, nalo wameshindwa kuthibitisha .. nayo imekufa .. sana sana watu wamewaona wajinga kwasababu unapomnyoshea mtu kidole kuwa kabebelewa au kalipwa hali anajijua kaenda kwa mapenzi yake na gharama zake anakuona mjinga. Na ndivyo wazushi hawa walivyoonekana na wanavyoonekana wajinga mbele ya malaki kwa mamilioni ya watanzania wanaojaa kwenye mikutano ya Lowassa.
Hoja yao ya muda Mrefu Lowassa Fisadi, wameshindwa kuithibitisha .. nayo imekufa. Hoja hizi zimekufa kwasababu ni hoja za kutungwa hazina ukweli, ni hoja za uongo, ni hoja za kutegenezwa.
Wakaja na Uzuhushi kuwa Dr. Mwakyembe ameandika waraka, Mwakyembe akajitokeza na kukanusha Uongo huo, wakaumbuka, uongo huo nao ukafa. Wakaja na uzuhushi wa tamko la jumuia ya nchi za Ulaya kuwa hawamtaki Lowassa, Jumuia hiyo imejitokeza na kukanusha .. wakaumbuka, uongo huo nao Ukafa,.
Kabla ya hapo walikuja na uzushi wa waraka wa Mungai kuwa anakanusha Shule za Sekondari hazikujengwa kwa juhudi za Lowassa bali alijenga yeye wakati wa Serikali ya awamu ya tatu .. ingawa Mungai hakujitokeza hadharani kukanusha ..taarifa nilizonazo Mungai hakuandika waraka ule, na Arusha siku ya lowassa anatangaza nia tulikuwa nae kwasababu yeye pia ni amehesabiwa, wameumbuka… uzushi huo nao umekufa.
Watanzania wanampenda zaidi Lowassa sasa hivi kwasababu kubwa mbili, kwanza wanajua na kuuhitaji uwezo wake mkubwa wa kazi, wanajua maendeleo makubwa aliyeleta, pili wameona anaonewa kwa kuzushiwa uongo wa kila aina, na ni hulka ya wanadamu kuwa upande wa mtu anayeonewa.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Edward Ngoyai Lowassa
Uchambuzi Umeandaliwa na Jacob Malihoja
Mwanaharakati
Nb: Usikose sehemu ya pili, ambayo ni muhimu zaidi kuijua
0 comments :
Post a Comment