Mahakama ya juu nchini Marekani imetoa uamuzi uliompendelea mwanamke mmoja wa kiislamu ambaye alienda mahakamani baada ya kunyimwa kazi katika kiwanda cha kushona nguo kutokana na vazi lake la hijab.
Kampuni hiyo ilikataa kumuajiri Samantha Elauf mwaka 2008 kama msaidizi wa mauzo kwa kuwa vazi lake la hijab lilikuwa linakiuka sera za kampuni hiyo ambayo ilikuwa inapinga wafanyikazi kuvaa kitu chochote kichwani.
Elauf hakuelezwa kuhusu sera hiyo ya mavazi.
Elauf aliwasilisha malalamishi yake na tume ya kuhakikisha kuwa kuna usawa wa utoaji wa ajira.
Katika ya kura 8-1,majaji hao walitoa ushindi dhidi ya kampuni ya Abercrombie and fitch kwa niaba ya mtafuta ajira samantha Elauf
0 comments :
Post a Comment